WATU watatu
waemefariki dunia katika matukio tofauti likiwamo tukio la mtu anaejulikana kwa
jina la Roza Mazengo alifariki dunia alipokuwa akiogelea katika bwawa la Mtera
.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya
saa tisa alasiri maeneo ya kambi ya
uvuvi Changarawe katika bwawa la Mtera.
Kamanda alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni ni baada
ya kuzidiwa na maji wakati akiogelea na tukio hilo lilitokea katika kijiji cha
Mgori kata ya Migori wilaya ya Iringa
vijijini.
Tukio lingine
lilitokea katika kijiji cha Lulaka wilaya ya Kilolo mtu aliye julikana
kwa jina la Kwinindo Mwalusamba mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kijiji cha Lukani alifariki
dunia kuangukiwana mti aliokuwa akiukata
kwa ajiri ya nguzo ya umeme.
Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba katika
hospital ya wilay wakati akiendelea na matibabu,
Wakati huo huo katika maeneo ya Iguruba kitongoji cha boma la ng’ombe tarafa ya Isimani
Wilaya ya iringa vijijini mtu anayafahamika kwa jina la Majaliwa Bosco alifariki dunia mara baada ya kung’atwa na
nyuki alipokuwa anawarushia mawe juu ya mti chanzo kikiwa ni mchezo wa kitoto.
No comments:
Post a Comment