Sunday, May 25, 2014

Kiwele:NAHITAJI SH 3.6 MILIONI KUPATA TIBA YA TATIZO LINALONISIBU

                        MAKALA
Ukikutana naye mitaani ama nyumbani kwake akiwa amepumzika na hata kama utamkuta akifanya baadhi ya shughuli kwa lengo la kujipatia kipato kamwe huwezi kuadhani kama kijana huyo  Frank Kiwele (21) anatatizo lolote.
Nikijana mtulivu na mwenye sura ya ucheshi mda wote utakapokuwa amekaa naye na hata kuzungumza na,ni vigumu kuamini kama anakabiriwa na tattizo la kutwa na haja kubw ana ndogo  tatizo lililodumu tangu kuzaliwa kwake hadi sasa.
“Tatizo hili nimezaliwa nalo kwani katika sehemu ya kiuono unapoanzia uti wa mgongo ninauvimbe,wataalamu wanasema ndio unaosababisha uwepo wa tatizo hilo,kimsingi limenitesa sana limenitenga na jamii na marafiki kutokana na kutokwa na haja ndogo na kubwa  bila mufulililozo bila ya hata kujitambua.”anasema Kiwele.
Kiwele ni mtoto wa pili katika familia ya Eliuta Kiwele ambaye amefariki duniani miaka 7 (mwaka 2007 akitanguliwa na mama mazazi wa Frank ,Sarah Ngadango aliyefariki mwaka 2002.

Kwa kifupi kiwele anasumbuliwa na tatizo la viongu vinavyotumika kuzuia haja ndogo na kubwa kutoka kushindwa kufanya kazi.

Binafsi ninatoa shukurani zangu za dhati  kwa wale waliofanikiwa kuyasoma makala ya Frenk Kiwele (21)katika gazeti la Mwananchi Mwananchi Jumapili toleo la Mei 3 mwaka huu.

Wengi wamehamsika na kuanza kumchangia mungua awabariki sana na awazidishie pale palipopungua ombi langu naomba muendelea kumchangii ili pamoja tuweze kumrejeshea kijana huyu matumaini ya kufurahia maisha yake hapa duniani.

CHAI BORA MUFINDI INAVYONOGESHA KOMBE LA "MUUNGANO MUFINDI CUP"

 Mwakilishi wa timu ya Zamalek ya Njombe kulia Shukuru Millinga akionyesha moja ya jezi alizokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Uzalishaji cha Kampuni ya Chai Bora ya Mufindi Mkoani Iringa Petronilla Alphone kushoto kwenye wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Kiwanda cha Chai bora  Mjini Mafinga Wilayani Mufindi mkoani Iringa,katikati ni mratibu wa michuoano hiyo Daud Yasini
Viongozi wa kiwanda cha Chai bora,chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Mufindi,waratibu kombe la Muungano na wawakilishi wa timu washiriki wa kombe la muungano wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo iliyofanyika kwenye viwanja vya kiwanda hicho mjini Mafinga mkoani Iringa,waliosimama ni wawakilishi watimu washiriki.




                                                           HABARi
KOMBE la Muungano “Muungano Cup” ambalo limeanza kutimua vumbi katika Viwanja vya  Igowole  na kile cha Wambi katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa limepigwa jeki na kampuni ya  Chai Bora, kwa kupatiwa msaada wa jezi seti 6 pamoja na mipira 10 kwa ajili ya kuboresha mashindano hayo.
Akikabidhi jezi na mipira hiyo kwa mratibu wa mashindano hayo ya kombe la Muungano- Daud Yasin, mkuu wa idara ya uzalishaji wa Kampuni ya Chai Bora Petronilla Alphonce, alisema  lengo la msaada huo ni kuyafanya mashindano hayo kuwa na muonekano wa pekee, shughuli iliyofanyika katika uwanja wa Chai Bora mjini Mafinga,.
Petronida amesema vijana hao wanapaswa kujituma katika michezo ili kuonyesha vipaji  na uwezo nyanda za juu kusini, ikiwa pamoja na kutotumia vinywaji vyenye kileo ili kuwafanya wawe na nguvu imara.
Aidha amesema misaada hiyo imegharimu jumla ya shilingi Milioni 7.7  na kuwa kampuni kwa kutambua hilo imetoa msaada huo kwa wachezaji wote, na mchango huo ni katika kuunga mkono mashindano hayo kwa kuiwakirisha kampuni kwa kiwango cha hali ya juu.
“Kampuni kwa kuthamini michezo imeona ni vema itoe jezi seti 6 na Mipira kumi, vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 7.7,  mchango huu tulioutoa tunajua una manufaa na utatuletea ushindani  mkubwa”alisema Petronilla
Akipokea msaada huo mratibu wa mashindano hayo ya Kombe la Muungano Daud Yasin alisema  kampuni ya Chai imekuwa kiyadhamini mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka  1998.
Amewataka wachezaji kuthamini vifaa hivyo kwa ubora wake kwani vina ubora wa hali ya juu, na kuwa matumaini yake ni vilabu shiriki kufanya vyema ili kuitangaza kampuni hiyo kupitia michuano hiyo inayozishirikisha timu za mikoa ya nyanda za juu kusini.
Alisema  mashindano hayo ambayo yamezinduliwa Mei 24 katika uwanja wa shule ya msingi Igowole ambapo mashindano hayo yataendeshwa katika viwanja viwili,  kwa maana ya kiwanja cha wambi cha mjini Mafinga na kiwanja Igowole shule ya msingi,
Uwanja wa Igowole utachezewa na timu ya Mbeya city ya jijini Mbeya, Zamalek na timu ya Igowole   sekondari,  huku mjini Mafinga katika uwanja wa Wambi kutakuwa na mechi ya timu ya Benk ya wananchi Mucoba, timu ya chuo cha Incoment na timu ya Black Cheeter ya mjini Iringa.
Amesema timu ya Mbaspo ambayo ni mabingwa watetezi waliochukua kombe la Muungano mwaka 2013 wamepewa fulsa ya kuingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali, ambapo amewataka wapenzi wa soka na mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia vipaji vya vijana wa nyanda za juu kusini.
Hata hivyo alisema mashindano hayo yamekuwa na msisimko kwa kuwa yanahusisha vijana walio na umri chini ya miaka 20, huku akiwataka wapenzi na mashabiki wa nyanda za juu kusini, kujitokeza kwa wingi kutazama vipaji vya vijana wa nyanda za juu kusini.
Daud Yasini alisema kwa mwaka huu  niwa mwisho kwake kuratibu mashindano ya kombe la Muungano kwani anastaafu na kuwa bingwa atachukua Kombe hilo moja kwa moja, kama ni kumbukumbu kwa timu ya uratibu wake wa mashindano hayo.
Yasini alisema  mashindano hayo yatakamilika  Juni 11 mwaka huu ambapo fainali ya kombe hilo mchezo wake utakachezwa katika uwanja wa Wambi wa mjini Mafinga.
MWISHO

MICHUANO KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI

Mkuu wa kitengo cha uzalishaji wa kampuni ya Chai bora ya Mufindi makoani Iringa Petronilla Alphoce akipena mkono na

Lambardo Mvanda, mwakirishi wa timu ya Black Cheeter ya Iringa mjini  wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msada wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Sh 7.7 milioni,Katikati mratibu wa mashindano hayo Daud Yasini