Timu ya Mpira wa Miguu ya Mkoani Iringa Lipuli inatarajia kurudi tena katika ulimwengu wa soka baada ya kufanikiwa kununua nafasi ya daraja la kwanza Tanzania bara iliyokuwa ikishikiliwa na timu ya Polisi mkoani hapa.
Taratibu za kununua time zimekamilika leo wakati Mdhamini Mkuu wa Timu hiyo Jesca Msambatavangu alipokabidhi Sh 14.5 milioni kwa ajili ya kuwasilisha malipo ya awali ya ununuzi wa timu hiyo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Iringa (IREFA)kutangza zabuni ya kuuzw akwa timu hiyo ambayo gharama za jumula zilikuwa Sh 20.5milioni.
Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha katika hafla iliyofanyika leo asubuhi Rais wa timu Jesca alisema lengo la mkakati huo ni kukuza mchezi wa mpira wa miguu mkoani hapa.
Alisema baada ya kukamilika kwamchakato wa kwanza kazi itakayofuata ni kupanga safi ya uongozi,kuajiri kocha bora na kusajili kikosi kitachaosaidia kuipandishi timu hiyo ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara katika msimo ujao wa ligi.
Awali mwenyekiti wa Timu hiyo Abuu Changawa aliuelezea mafanikia ya mchakato huo kuwa ni sehemu muhimu katika kufanyamapinduzi ya soka mkoani hapa.
"Kwa muda mrefu tumekuwa tuhakihangaika kutaka kupandisha timu bila mafanikio,lakini hatua ya leo ni nzuri na nisema tumefurahi kuipata nafasi hii na tutahakikisha tunafanikiwa kufikia Ligi Kuu ya Vodacom msimo ujao"alisema Changawa
No comments:
Post a Comment