Thursday, June 12, 2014

FRANK KIWELE AWASHUKURU WALIOMCHANGIA

 

MMILIKI WA MTANDAO HUU KATIKATI  KULIA GEOFREY NYANG'ORO KATIKATI AKIMKABIDHI FEDHA ZA MSAADA FRANK KIWELE (21) FEDHA HIZO ZIMETOLEWA NA WASOMJA WA GAZETI LA MWANANCHI NA MCHANGO HUU NI KWAAJILI YA KUCHANGIA  GHARAMA ZA MATIBABU YA TATIZO LINALOMSUMBUA  TANGU KUZALIWA KWAKE

 WANAOSHUHUDI TUKIO HILO  KUSHOTO NA AFISA USTAWI WA JAMII MKUU WA MANISPAA YA IRINGA GASPER NSANYE NA KULIA NI MJOMBO WA KIJANA HUYO THOMAS NGANDANGO

 


 

HABARI



Iringa.Kijana Frenk Kiwele anayekabiliwa na tatizo la kutokwa na haja kubwa na ndogo mfulilizo amepkea msaada wa Sh 510,000 kutoka kwa wasomaji wa gazeti la Mwananchi na kudai sasa anapata matumaini ya kupona tatizo lake.

Kiwele alikabidhiwa fedha hizo juzi na mwandishi wa gazeti la Mwananchi  mkoani hapa  Geofrey Nyang’oro ambaye pia ndiye mmiliki wa mtandao huu,hafla hiyon amefanyika nyumbani kwake Kinegamgosi A  kata ya Ruaha ndani ya Mansipaa ya Iringa.

Hafla hiyo imeshuhudiwa na  Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu wa Manispaa ya Iringa Gasper Nsanye na Mjomba wa kijana huyo Thomas Ngandango.

Akizungumza muda mufi baada ya kukabidhiwa fedha hizo  Frank aliwashukuru wasomaji wa Gazeti hilo  kwa kumchangia kiasi hicho cha fedha baada ya kusoma makala hiyo licha ya kuwa hawamjui na kudai mungu atawazidisha pale walipopungukiwa.

 Kwa mjibu wa taarifa ya madakati Bingwa kutoka Hosptali ya Taifa ya Muhimbili waliofanya uchunguzi wa tatizo lake wanadai gharama zinazohitajika kwa ajili ya matibabu ya Farnk Kiwele ni  Sh 3,650,750

Kwa upande wake Afisa Usitawi wa Jamii Mkuu wa Manispaa ya Iringa Gasper Nsanye amemshukuru mwandishi wa makala hayo, kampuni ya Mwananchi Communicationi LTD ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi,Thecitizen na Mwanaspoti kwa kukubali  kuchapisha makala hayao gazeti jambo liliwafanya wasomaji wake kuoisoma na kutoa kiasi hicho cha fedha.

 “Mini nianze kwa kumshukuru mwandishi wa makala haya,nilishukuru kampuni ya Mwananchi Communication LTD na pia wasomaji wa gazeti la Mwananchi kwa mchango wao,ofisi yetu inashughulikia suala hilo kw akaribu na hivi sasa tumefungua kitabu cha Benki katikA Benki ya NMB chenye akaunti namba ya FRANK ELIUTA KIWELE  A/C NO 16110000481”alisema Nsanye na kuongeza:

“Katika A/C hiyo kwenye kikao cha wakuu wa Idara na waheshimiw amadiwani wa Manispaa ya Iringa walichangia Sh 150,000 huku wadau wengine wa mkoani hapa wakitoa mchangia wa Sh 50 000 na kufanya jumla ya Sh 200,000 na kwa sasa tukichanganya na hizo tutakuwa na Sh 700,000”alisema Nsanye.

Nsanye alisema bado michango inahitajika kufikia kiwango kinachohitajika na kuongeza kuwa hata uongozi wa Manispaa hiyo unaendelea na mchakato wa kuwafikia wadau mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha jukumu hilo.

Naye Mjumba wa Frank Thomas alitoa shukurani zake kwa makundi yote yalitoa mchango huo na kudai pindi kiasi hicho kitakapopatikana atakuwa bega kwa bega katika kuuguza mpya wake kazi aliyoifanya kw amda mrefu sasa.


MWISHO