Saturday, May 24, 2014

Lumiye: Tumeanzisha chama kupinga manyanyaso



Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) Ally Lumiye akizunguzunguza na wafugaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha mtakuja wilayani chunya jijini mbeya




                                                           HABARI

WAFUGAJI  kote nchini wameshauriwa kujiunga na Chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwamo vitendo vya unyanyasaji walivyodai wamekuwa wakitendewa na baadhi ya  viongozi na watendahi serikalini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa (CCWT) Taifa Ally Lumiye alipokuwa akizungumza na wafugaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mtakuja wilayani Chunya Jijini Mbeya .

Ally amesema  kwa muda mrefu jamii ya wafugaji imekuwa ikitendewa vitendo vya kinyama ikiwamo kuhamishwa katika maeneo yao bila ya kufuata taratibu na wakati mwingine mifugo kukamatwa huku wafugaji wakitozwa ushuru mkubwa kitendo kinachochangia kuwafilisi.

Amesema  ndani ya chama hicho wafugaji watapata fursa ya kutetewa pindi wanapofanyiwa vitendo vya uonevu kwakuwa kimeajiri wanasheria kwa ajili ya kazi hiyo.

“Chama chetu kimepata usajil Desemba mwaka jana,kama mnavyofahamu jamii ya wafugaji imekuwa kitendewa vitendo vya unyanyasaji ,wafugaji kuhamishwa bila kufuata utaratibu,mifugo kukamatwa na kuzwa faini  kubwa na hata wakati mwingine kutaifishwa…sasa wafugaji mmepata mtetezi wenu mtumieni”alisema  Lumiye na kuongeza  kuongeza:

“Kwa sasa chama chetu kimeajili wanasheria ambao  jukumu lao ni kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa wafugaji ili kuona kama kunawafugaji wametendewa vitendo vya ukiukwaji wa sheria hatua ziweze kuchukuliwa dhida ya wahusika”alisema.

No comments:

Post a Comment