Thursday, June 13, 2013

Watuta wafa kwa matukio tofauti Iringa


WATU  watatu waemefariki dunia katika matukio tofauti likiwamo tukio la mtu anaejulikana kwa jina la Roza Mazengo alifariki dunia alipokuwa akiogelea katika bwawa la Mtera .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tisa alasiri  maeneo ya kambi ya uvuvi Changarawe katika bwawa la Mtera.

Kamanda alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni ni baada ya kuzidiwa na maji wakati akiogelea na tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Mgori kata ya Migori  wilaya ya Iringa vijijini.

Tukio lingine  lilitokea katika kijiji cha Lulaka wilaya ya Kilolo mtu aliye julikana kwa jina la Kwinindo Mwalusamba mwenye umri wa miaka 19  mkazi wa kijiji cha Lukani alifariki dunia  kuangukiwana mti aliokuwa akiukata kwa ajiri ya nguzo ya umeme.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba katika hospital ya wilay wakati akiendelea na matibabu,

Wakati huo huo katika maeneo ya Iguruba  kitongoji cha boma la ng’ombe tarafa ya Isimani Wilaya ya iringa vijijini mtu anayafahamika kwa jina la Majaliwa Bosco  alifariki dunia mara baada ya kung’atwa na nyuki alipokuwa anawarushia mawe juu ya mti chanzo kikiwa ni mchezo wa kitoto.

Lipuli yafufuka sasa kushiriki daraja la kwanza ngazi ya taifa msimu ujao

Timu ya Mpira wa Miguu ya Mkoani Iringa Lipuli inatarajia kurudi tena katika ulimwengu wa soka baada ya kufanikiwa kununua nafasi ya daraja la kwanza Tanzania bara iliyokuwa ikishikiliwa na timu ya Polisi mkoani hapa.

Taratibu za kununua time zimekamilika leo wakati Mdhamini Mkuu wa Timu hiyo Jesca Msambatavangu alipokabidhi Sh 14.5 milioni kwa ajili ya kuwasilisha malipo ya awali ya ununuzi wa timu hiyo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia  Chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Iringa (IREFA)kutangza zabuni ya kuuzw akwa timu hiyo ambayo gharama za jumula zilikuwa Sh 20.5milioni.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha katika hafla iliyofanyika  leo asubuhi Rais wa timu Jesca alisema lengo la mkakati huo ni kukuza mchezi wa mpira wa miguu mkoani hapa.

Alisema baada ya kukamilika kwamchakato wa kwanza kazi itakayofuata ni kupanga safi ya uongozi,kuajiri kocha bora na kusajili kikosi kitachaosaidia kuipandishi timu hiyo ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara katika msimo ujao wa ligi.

Awali mwenyekiti wa Timu hiyo Abuu Changawa aliuelezea mafanikia ya mchakato huo kuwa ni sehemu muhimu katika kufanyamapinduzi ya soka mkoani hapa.

"Kwa muda mrefu tumekuwa tuhakihangaika kutaka kupandisha timu bila mafanikio,lakini hatua ya leo ni nzuri na nisema tumefurahi kuipata nafasi hii na tutahakikisha tunafanikiwa kufikia Ligi Kuu ya Vodacom msimo ujao"alisema Changawa

Finca yaburutwa CMA Iringa


 

WAFANYAKAZI 13 wa Kampuni ya Finca Tanzania (M.C.F) Ltd Tawi la Irimga waliofukuzwa kazi wanatarajia kuibuza kampuni hiyo katika baraza la Usuluhishi Tawi la Iringa (CMA).

Katibu wa TUICO Mkoa wa Iringa Magasa Chimola aliliambia gazeti hili jana kuwa wafanya kazi hao wlaifika katika ofisi hizo leo na kujaza fomu kwa ajili ya kufungua jarada hilo la kesi.

Kwa uapnde wao wafanya kazi hao walisema hatua ya kufungua shauri katika Tume ya usuluhishi ni kuhakikisha wanapata haki zao ambazo walidai zimekiukwa na kufukuzwa kwao ni kitendo cha uonevu.

Wafanyakazi hao wametaja  sababu za kufukuzwa  kwao  ikiwa ni siku moja tangu  kampuni hiyo kutangaza majina yao kwenye gazeti la Mwananchi  toleo la Julai 13 mwaka huu likiueleza umma kuwa kuanzia sasa watu hao si wafanya kazi wa Kampuni hiyo.

Walitaja sababu  hizo kuwa ni na kitendo chao  cha kuandika barua na kuituma kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo taifa Mei 16 mwaka huu wakiomba kukutana nae ili kutoa kero zao walizodai zilidumu kwa muda mrefu bila kushughulikiwa na uongozi wa Finca Tawi la Iringa na kanda.

“Kwa mda mrefu tumekuwa tukifanya kazi katika mazingira magumu,tulijaribu kuwasiliana na uongozi wa  tawi  na kanda lakini jitihadi zetu hazikuzaa matunda,na tuliamua kuwasilisha taarifa zetu ngazi za juu na badala ya kutusikiliza madai yetu tulipata barua siku ile ile ya ikitutisha vitisho kutoka kwa Mkurugenzi wetu Taifa”alisema Mmoja wa wafanya kazi hao.

Kero nyiungine walizoziainisha ni pamoja na wafanyakazi kuchelewa kuthibitishw akazini,kucheleweshwa kwa mikopo kwa miezi mingi bila kupewa sababu toka kwa uongozi tawi,wafanyakazi kuwajibika kutoa majibu katika makosa ambayo hawakutenda,kamati ya maadili kuendeshwa kibabe na wafanyakazi kuingia gharama binafsi kufanya kazi za Kampuni.

Wafanya kazi waliotangazw akufukuzwa kazi ni pamoja na Anderw Sharaj, Aneth Shirima,Bony Msindo,Cotrida Mtweve,Damian Msanganzila,Edoxia Mbwilo,Happy Sanga na Mgewa Mbondo.

Wengine ni Mihayo Stepheno,Peter Zephania,Widman Masika ,Hennry Martin na Calvin Mlokozi