WAFANYAKAZI 13 wa Kampuni ya Finca Tanzania (M.C.F) Ltd Tawi
la Irimga waliofukuzwa kazi wanatarajia kuibuza kampuni hiyo katika baraza la
Usuluhishi Tawi la Iringa (CMA).
Katibu wa TUICO Mkoa wa Iringa Magasa Chimola aliliambia
gazeti hili jana kuwa wafanya kazi hao wlaifika katika ofisi hizo leo na kujaza
fomu kwa ajili ya kufungua jarada hilo la kesi.
Kwa uapnde wao wafanya kazi hao walisema hatua ya kufungua
shauri katika Tume ya usuluhishi ni kuhakikisha wanapata haki zao ambazo
walidai zimekiukwa na kufukuzwa kwao ni kitendo cha uonevu.
Wafanyakazi hao wametaja
sababu za kufukuzwa kwao ikiwa ni siku moja tangu kampuni hiyo kutangaza majina yao kwenye
gazeti la Mwananchi toleo la Julai 13
mwaka huu likiueleza umma kuwa kuanzia sasa watu hao si wafanya kazi wa Kampuni
hiyo.
Walitaja sababu hizo
kuwa ni na kitendo chao cha kuandika
barua na kuituma kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo taifa Mei 16 mwaka huu
wakiomba kukutana nae ili kutoa kero zao walizodai zilidumu kwa muda mrefu bila
kushughulikiwa na uongozi wa Finca Tawi la Iringa na kanda.
“Kwa mda mrefu tumekuwa tukifanya kazi katika mazingira
magumu,tulijaribu kuwasiliana na uongozi wa tawi na
kanda lakini jitihadi zetu hazikuzaa matunda,na tuliamua kuwasilisha taarifa
zetu ngazi za juu na badala ya kutusikiliza madai yetu tulipata barua siku ile
ile ya ikitutisha vitisho kutoka kwa Mkurugenzi wetu Taifa”alisema Mmoja wa
wafanya kazi hao.
Kero nyiungine walizoziainisha ni pamoja na wafanyakazi
kuchelewa kuthibitishw akazini,kucheleweshwa kwa mikopo kwa miezi mingi bila
kupewa sababu toka kwa uongozi tawi,wafanyakazi kuwajibika kutoa majibu katika
makosa ambayo hawakutenda,kamati ya maadili kuendeshwa kibabe na wafanyakazi
kuingia gharama binafsi kufanya kazi za Kampuni.
Wafanya kazi waliotangazw akufukuzwa kazi ni pamoja na
Anderw Sharaj, Aneth Shirima,Bony Msindo,Cotrida Mtweve,Damian Msanganzila,Edoxia
Mbwilo,Happy Sanga na Mgewa Mbondo.
Wengine ni Mihayo Stepheno,Peter Zephania,Widman Masika ,Hennry
Martin na Calvin Mlokozi
No comments:
Post a Comment