Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) Ally Lumiye akizunguzunguza na wafugaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha mtakuja wilayani chunya jijini mbeya
HABARI
WAFUGAJI kote nchini wameshauriwa kujiunga na Chama cha
wafugaji Tanzania (CCWT) ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwamo vitendo vya unyanyasaji walivyodai wamekuwa wakitendewa
na baadhi ya viongozi na watendahi serikalini.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti
wa (CCWT) Taifa Ally Lumiye alipokuwa akizungumza na wafugaji kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mtakuja wilayani Chunya Jijini Mbeya .
Ally amesema kwa muda mrefu
jamii ya wafugaji imekuwa ikitendewa vitendo vya kinyama ikiwamo kuhamishwa
katika maeneo yao bila ya kufuata taratibu na wakati mwingine mifugo kukamatwa
huku wafugaji wakitozwa ushuru mkubwa kitendo kinachochangia kuwafilisi.
Amesema ndani ya chama hicho
wafugaji watapata fursa ya kutetewa pindi wanapofanyiwa vitendo vya uonevu
kwakuwa kimeajiri wanasheria kwa ajili ya kazi hiyo.
“Chama chetu kimepata usajil Desemba
mwaka jana,kama mnavyofahamu jamii ya wafugaji imekuwa kitendewa vitendo vya
unyanyasaji ,wafugaji kuhamishwa bila kufuata utaratibu,mifugo kukamatwa na
kuzwa faini kubwa na hata wakati mwingine kutaifishwa…sasa wafugaji mmepata
mtetezi wenu mtumieni”alisema Lumiye na kuongeza kuongeza:
“Kwa
sasa chama chetu kimeajili wanasheria ambao jukumu lao ni kukusanya taarifa
mbalimbali kutoka kwa wafugaji ili kuona kama kunawafugaji wametendewa vitendo
vya ukiukwaji wa sheria hatua ziweze kuchukuliwa dhida ya wahusika”alisema.
