Rais Jakaya Kikwete amekipeana mkono na mmoja wa wajumbe wa jumuiya ya Madaktari walifika Ikulu kuitikia wito wa Rais kikwete kujadili maandamano
Suluhu ya mgomo
HUKU maisha ya watanzania wagonjwa na wale wanaouguza ndugu zao wakiendelea kukata tamaa ya maisha kufuatia kukosa huduma zinazotokana na mgomo wa madaktari unaoingia siku ya tatu leo,Rais Jakaya Kikwete amewaita madaktari hao Ikulu.
Hatua ya Rais Kikwete imekuja ikiwa ni siku moja tu tangua Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuahirisha ziara ya iliyokuwa aifanye kwa muda wa siku 10 Mkoani Mwanza lengo likiwa kushughulikia mgomo huo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa Nchi kujitosa katika mgogoro huo mkubwa kupata kutokea tangu uatwala wake wa awamu ya pili uingie madakrakani.
Awali alitangazwa kuwa Rais Kikwete alitaraji kuzungumza na Wananchi kupitia vyombo vya habari leo majira ya saa kumi jioni ambapo angehutubia wazee wa jiji la Dar es Salaam lakini ghafla suala hilo likaahirishwa na kisha kuamua kukutana na Madaktari.
Huenda mazungumzo yake na Madaktari yakaleta suruhu ya kudumu ya mgogoro ambao hadi sasa umesababisha athari na usumbufu kwa baabdhi ya watu ambao dnugu zao wamelazwa hospitalini.
Wakati Rais Kikwete akikutana na uongozi wa Madaktari hao hali katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),Taasisi ya Mifupa (MOI) na hosptali nyingine jijini Dar es Salaam huduma zilikuwa zimezorota.
Mgomo unafanyika wakati ambapo hivi karibuni Rais Kikwete aliwapa pole umma wa watanzani kutokana na mgomo uliositishwa Februari 9 mwaka huu kufuatia kikao cha Maridhiano baina ya Madaktari na Waziri Mkuu na kudai kuwa serikali itahakikisha hilo halijirudii.
