Monday, March 5, 2012

MAWAZIRI WAJIFUNGIA OFISNI KUKWEPA WAANDISHI WA HABARI

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda kulia ni Naibu wake Dk Lucy Nkya

Kufuatia tishio la mgomo wa madaktari

WAKATI Madaktari wakitarajia kuanza mgomo kesho  wa kushinikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda na Naibu wake Dk Lucy Nkya kujiuzulu,mawaziri hao jana walijifungua ofisini kwao kutwa nzima wakikwepa kuzungumza na waandishi wa habari.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Madaktari walitoa tamko zito la  kuitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha vigogo hao wakisiasa kabla ya Jumatano wiki hii la la sivyo watagoma kufanya kazi.
 Madaktari wanawatuhumu kuwa viongozi hao ni chanzo cha mgomo uliotangazwa Januari 23 ambao ulisababisha vifo vya watu kadhaa na wenginewengi kuathirika kwa kile walichadai walishindwa kutimiza wajibu wao.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walifika katika ofisi za Maziri hao  mapema asubuhi wakita kujua msimamo wa vigogo hao wa kisiasa katika Wizara ya Afya juu ya tamko la Madaktari
Hata hivyo wanahabari haop kwa nyakati tofauti walikutana na wasaidizi wa mawaziri hao walidai vigogo hao hawako tayari kuzungumza na waandishi wa habari.
Katika Ofisi ya Waziri Mponda wanahabari walielezwa kuwa Waziri hayuko tayari kuzungumzia suala hilo kwa sababu liko juu ya uwezo wake.
“Nataka mfahamu kuwa waziri anajua uwepo wenu lakini hayuko tayari leo kuzungumza na waandishi wa habari,hawezi kuzungumzia suala hilo sababu lipom juu yab uwezo wake”alisema Mmoja wa maofisa katika ofisi ya Waziri Mponda.
Pia katika Ofisi ya Naibu waziri wa Wizara hiyo Dk Nkya waandishi walipoingia walikutana na mmoja wa wasaidizi ambaye alitoa kauli kama ya mtangulizi wake.
Baada ya waandishi kusubiri kwa muda mlefu,ilipofika saa saba mchana Ofisa katika Ofisi ya Waziri wa Afya ,aliwaeleza kuwa angerudi tena ofisini kumshauri Waziri Mponda atoke ili aweze kuzungumza na wandishi hao.
Lakini baada ya muda alitoka Msemaji wa Wizara hiyo aliyekuwa kwenye mkutabno wa wakurugenzi wa Idara zote za Wizara ya Afya Nsachris Mwamwaja  na kusisitiza kuwa mawaziri hawakuwa na cha kusema ju ya suala hilo sababu liko juu ya uwezo wao.
“Suala la madaktari linajadiliwa katika ngazi za juu,Mawaziri hawawezi kutoa maoni wala tamko lolote juu ya jambo hili”alisisitiza Mwamaja.


Mwamaja alisema suala hilo kwa sasa liko juu ya uwezo wa mawaziri hao na kusisitiza hawawezi kusema chochote huku akishauri waandishi kufuatilia ngazi za juu.
Msimamo wa Madaktari
Rais wa chama cha Madaktari Tanzania MAT Dk Namala Mkopi aliliambia Mwananchi kuwa msimamo wa madaktari upo palepale wa kutoendelea kufanya kazi endapo mawaziri hawatajiuzulu.
“Madaktari walishapitisha hili kwenye kikao chao,msimamo wao ni uleule kwamba wao hawataendelea kufanya kazi,ikiwa mawaziri hao watakuwa hawajajiuzulu ifikapo jumatano (kesho).

Wizarani
Wakati hali ikiwa hivyo,jana ukumbi wa mikuatno wa Wizara ya Afya ulitawaliwa na vikoa vya mda mrefu vilivyohusisha wakurugenzi wote wa idara za wizara ya Afya.
Habari za ndani zinasema wakurugenzi hao walikutana kujadili sakata hilo la madaktari na namna watakapokabiliana na tisho la mgomo huo mpya.
“Wakurugenzi wote wa Idara za Wizara wapo ndani ya kikao na wananendelea na mkutano chini ya Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk Dolnald Mbando,wanajadili suala la Madaktari,wanatafuta  namna watakavyokabiliana na tishio la mgomo huo mpya ”kilisema chanzo hicho.
Akizunguzia hilo Mwamaja alikiri kuwepo kwa kikao hicho lakini akabainisha kuwa kilikuwa cha uongozi wa Wizara na walikuwa wakijadili masuala mbalimbali na si kuhusu mgogoro wa madaktari.
“Nikweli kulikuwa na kikao hapa wizarani,hiki ni cha menejimenti walikutana kujadili mambo mbalimbali lakini hayahusiani na mgogorowa madaktari”alisema Mwamaja.
Kuhusu waziri na Naibu wake
Habari za ndani zinasema vigogo hao wateule wa rais hawana mpango wowote wa kujiuzulu.
Kwa mjibu wa mtoa habari hawana wasiwasi na tisho hilo sababu wanaamini madaktari hawatagoma bali wanatishio tu.
“Awali tulipata taarifa za wao kutaka kujiuzulu,lakini inasemekana kwa sasa hawana mpango huo na wanadai tamko la madaktari ni kutishia tu na wala hawawezi kugoma”kilisema chazno hicho.

SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI SEHEMU YA KWANZA

 Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari.Dk Stephen Ulimboka kabla ya kuanza kwa mkutano wa maridhiano ya kumaliza mgomo wa madaktari,Dk Ulimboka ni
                                   Waziri wa Afya na Usatawi wa Jamii Dk Hadji Mponda
ULIKUWA MGOMO WA KIHISTORIA
Wengi wanasema haijawahi tokea

JANUARI 23 mwaka huu  saa 11:30 jioni Dk Stephen Ulimboka mwenyekiti wa jumiya ya Madaktari akatangaza mgomo wa madaktari wenye lengo la kuishinikiza serikali kutekeleza madai yao.
Kutangazwa kwa mgomo kulikofanywa  na  jumuiya ya hiyo  kumekuja baada ya vikao vizito vilivyofanywa na madaktari hao  vikongozwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT)kushindwa kuzaa matanda.
Intenship chanzo cha mgogomo
Hilo haliwezi kukwepeka sababu chanzo cha mikutano ya madaktari ilitokana na hatua zilichukuliwa na serikali dhidi ya Madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili kutimuliwa katika vituo vyao vya kazi na kurejeshwa wizarani.
Madaktari hao ambao idadi kamili imekuwa ikishindw kujulikana kufuatia taarifa za awali kudai ni 225 huku habari toka wizarani zikidai ni 197 walitimuliwa na uongozi wa hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwakile kilichoelezwa ni kukiuka mkataba waliongia baina yao na uongozi wa hosptali hiyo.
Mmoja ya vipengele vya mkataba kinaeleza bayana kuwa ni marufuku kwa Interns kugoma wala kushawishi mgomo  kwa kipindi chote atakachokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.
Lakini wanataalam hao waligoma kwa muda wa siku mbili mfuliluzo kati ya  Januari 3 na 4 wakishinikiza serikali kuwalipa posho zao za miezi miwili zilizokuwa zimecheleweshwa.


Kwa muda wa simu mbili Mgomo uliotangazwa na Jumiya hiyo unadaiwa ni kutokana na hatua zilichukuliwa na lizochukuliwa madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili ambao walitimuliwa na uongozi wa Hosptali hiyo baada ya kuendesha mgomo wa siku mbili wakidai  posho zao za miezi miwili.
Idadi ya madaktari hao waliogoma Januari 2 mwaka huu ilikuwa na utata baada ya taarifa za awali zilitolewana uongozi wao kueleza kuwa walikuwa 225 huku tamko la serikali kupitia kwa Naibu waziri wa afya Dk Lucy Nkya ikisema ni 194.
Habari zuilieleza kuwa Madaktari hao walitimuliwa siku moja baada ya kulipw fedha zao ambapo uongozi walipowasili Hosptalini walikumbana na barua iliyowataka kuacha kazi na kurejea Wizarani.
Kufuatia hatua hiyo Junauri 12 mwaka huu  Chama cha Maktari Tanzania MAT kiliitisha mkutano wa dhararu wa baraza kuu na kujdali hoja kadhaa huku kikiipa serikali saa 72 kwa serikali kuwarejesha madaktari waliokuwa katika mafunzo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika tamko lao hilo Madaktari walielezea kuwa kufukuzwa kwa madaktari hao ni ukiukwaji wa haki za binadamu sababu wao walioshindw akuwalipa fedha zao ndio waliotenda kosa na hao ndio waliostahili adhabu
Baraza hilo la dhararua pia lilielezea dhamira ya kuendelea na mkutano wa Madaktari wote siku Juari 18 na kujadili mada mbalimbali ikiwamo ya hatima ya fya ya mtanzania na mazingira bora ya kazi
Majibu ya Wizara
Siku mbili baadaye,Januri 17 Wazira kupitia kwa Naibu waziri wa Afya  Dk Lucy Nkya ilitoa tamko lilipuuza madai ya madaktari hao huku likifafanua sababu za kuwatimua katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili kuwa ni kutokana na madaktari hao kuvunja mkataba na mwaajiri wao.
“Ieleweke kuwamba wataalamu hawa huingia mikataba na hosptali husika,mkataba wanaoingia umeainisha kwamba hawatagoma au kuanzisha mgomo”alisema Naibu waziri katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Dk Nkya alifafanua sababu za kuwatawanya katika vituo mbalimbali madaktari hao kuwa ilitokanana tathimini  iliyofanywa na wizara ambayo ilibaini kuwapo kwa idadi kubwa ya madaktari wa mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika mkutano huo pia Naibu waziri huyo alifafanua kuwa MAT ni miongoni mwa vyama vingine vya hiyari katika sekta ya Afya ambavyo kazi zake ni kufuatilia masuala ya wanachama wao kwa kutumia mifumo iliyowekwa  kisheria.
Dk Nkya alisema  wataalamu wote katika sekta ya afya katika husimamiwa na mabaraza ya Kitaaluma ambayo ni mamlaka  zilizoanzishwa kwa sheria za bunge.
Alisema mabaraza hayo ndiyo yenye dhamana kusimamia ufanisi wa mazoezi kwa vitendo na wahusika huku aitaka MAT kufanya kazi na Wizara iko tayari kushirikiana nao katika masuala yenye kuwezesha kuboresha huduma za afya.
Alionya na kukumbusha chama hicho kutekeleza majukumu yake kwa mjibhu wa katiba ya chama hicho kwa kushirikiana na serikali katika kuimarisha sekta ya afya na wataalamu walio kwenye sekta hiyo kwa manufaa ya nchi badala ya kujihusisha na harakati.
Tamko la Wizara  lawatibua  Madaktari
Katika mkutano wao wa Januri 18 mwaka huu Madakatari walisema majibu ya Wizara ya kudai madai yao hayana msingi ni ya kisiasa na yakuidhalisha taalamu yao.
Madaktari hao waliokutana katika ukumbi wa Rusian walikubaliana kutuma ujumbe wa watau watatu ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Chama hicho Dk Primus Saidia kwenda wizarani kumuita naibu huyo kwenye mkutano wao.
Hatua ya kumuita Naibu waziri huyo ililenga kupatikana kwa majibu ya maswali yao mengiambayo katika mkutano huo waliibua hoja nne na kuzijadili huku wakieleza kuwa suala la madaktari waliokuwa katikamafunzo ya vitendo lilikuwa linasubiri uamuzi baada ya serikali kushindwa kutekeleza madai yao  kwa muda uliokuwa umepangwa.
Ombi la kukutana na Naibu Waziri wa afya
Ujumbe toka Wizarani ulirejea na majibu kuwa Naibu huyo wawaziri alikuwa amekubaru kufika katika ukumbi wa mikutano wao lakini akaomba muda wa saa moja ili aweze kuwasilisna na wasaidizi wake.
Wakati Dk Saidia alikitoa taarifa hiyo,ghafla  alipoke simu na kutoka nje ya ukumbi na aliporejea aliwaeleza washiriki wa mkutano zaidi ya 200 waliokuwa wamejipanga kusikiliza naibu waziri huyo na kusema,
“Naibu waziri ameweataka radhi ninyi wote na kueleza kuwa hatakuja kwenye mkutanona badala yake tutakutana nae kesho saa nane mchana”alisema Saidia.
Chenga zikaanza
Siku ya pili ya mkutano Alhamisi ya Januari 19 Madaktari zaidi ya 300 walikusanyika mapema asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Don Bosco wakisubiri ujio wa Naibu waziri huyo wa Afya DK Lucy Nkya.
Wakati wao wakikusanyika ujumbe wa watu watatu ukiongozwa na Makamu wa Rais uliwasilisha barua pamoja na mihitasari ya vikao  na madai yao ya jumula na mahali wanapofanyia mkutano.
Wajumbe hao waliporudi walikuja na taarifa za Naibu waziri huyo kukataa kukutana na Madaktari katika ukumbi ulioandaliwa nao na badala yake wizara ingeandaa ukumbi  mwingine.
Madaktari walipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kilikuwa ni matumizi mabaya ya fedha sababu wao walikuwa tayari wamelipia ukumbi huo,lakini pia wakadai tukio hilo lingesababisha usumbufu kwao.
Wakiwa bado kwenye chumba hicho madaktari hao ghafla walielezwa tayari ukumbi ulikuwa umepatikana ambao ni Arnatoglo na kuwataka wao kwenda katika ukumbi huo kwa muda wa nusu saa vinginevyo Waziri huyo na ujumbe wake angeondoka.

Madaktari waligoma kwenda kwenye ukumbi huo kwa kile walichodai kuwa ni umbali wa kutoka eneo walipo na kwamba kutokana na hali ya usafiri ilivyokuwa muda wa nusu saa usingetosha kumkuta DK Nkya akiwa kwenye chumba cha mkutano.
Pia Dk Saidia alisema kundi la madaktari hao lingeonyesha taswira ya maandamano jambo ambalo lingesababisha usumbufu kwa wananchi wanaotumia njia hizo na pia kuhofia uwezekano wa Madaktari hao kukamatwa na Polisi kwa kisingizio cha kuandamana bila kibali.
Aidha madaktari hao wakasema Naibu waziri huyo ameonyesha dhararu kwa kitendo chake cha kwenda ukumbi mwingine ilihali akijua watu wako sehemu nyingine.

“Nirahisi kwa yeye kuja kuliko umati wa watu 300 kujaa barabarani kwa lengo la kumfuata,lakini kwanini ameenda Arnatouglo hali akijua watu wako huku,hii ni dhararu”alisema mmoja wa madaktari alipochangia kwenye mkutano wao.
Kufuatia mvutano huo Madaktari waligoma na kuweka azimoa la kukutana siku ya pili katika mwenndelezo wa mkutano wao huku wakiwa na wazo la kuona mamlaka nyingine za juu.

Kwa upande wake kutokana na mvutano huo Dk Nkya alikaririwa na vyombo vya habri akisema asingewasikiliza tena Madaktari na kuwataka madai yao yafikishwe serikalini kwa kutumia Shirikisho la vyama vya Serikali kuu na Afya (TUGHE) ambao wapo kisheria kushughulikia madai hayo.

"Madaktari hawa wameonyesha kiburi,kuanzia sasa sitawasikiliza na badala yake madai yao yote yawasilishwe wizarani kupitia Tughe na kama wataaendelea na vikao vyoa mfululizo kwa siku saba nitawafukuza"anasema Dk Nkya.


Harakati za kumona Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Siku iliyofuata Madaktari hao walikutana tena katika ukumbi wa mikutano wa Don Bosco na kudhamilia kumuona Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Madaktari huku wakiwa na imani kubwa na Waziri Mkuu walikubalina kuorodhesha madai yao na kuwasilisha kwake ili kutafuta ufumbuzi wa madai hayo huku wakitupia lawama watendaji wa wizara kuwa hawana nia thabiti ya kutatua madai yao.
Asubuhi na Mapema siku ya Ijumaa Januari 21 ujumbe wa watu watatu ukiongozwa na Rais wa MAT Dk Namala Mkopi,uliwasili Ofisini kwa Pinda na kutoa mapendekezo ya madaktari kutaka kuonana nae.
Hata hivyo safari hii dhamira yao haikutimia baada ya wajumbe hao kuelezwa na wasaidizi wa Pinda kuwa alikuwa safarini kuelekea Arusha.
Wajumbe aho waliwaambia wajumbe wa  mkutano kuwa pamoja na Pinda kuwa safarini kuelekea Arusha bado wangepata jibu la hitaji lao kabla ya saa kumi jioni.
Mwilikilishi wa Pinda awatibua
Huku akionysha hali ya huzuni makamu wa Rais Dk Saidia alisema “Ujumbe uliokwenda kwa pinda umerudi lakini majibu yaliyopatikana huku yamekatisha tamaa washiriki wa mkutano”
Namala alitoa kauli hiyo majira ya saa tatu usiku alipowasiliana kwa njian ya simu na mwanadishi wa makala haya.
Alisema kufautia kauli hiyo washiriki walifikia hatua ya kufanya uamuzi mbya lakini kukafanyika kazi ya ziada ya kuwatuliza.
Alisema pamoja na hatua hiyo wajumbe walikubaliana kukutana tena Jumatatu ya Januari 23 ambapo wangekubaliana hatua za kuchukua.
Siku tanotangu kutangazwa kwa mgomo
Jumanne ya Januri 24 ndio siku ya kwanza ya kuanza kwa mgomo wa madaktari na katika athari zilianza kujitokeza moja kwa moja katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.