MMILIKI WA MTANDAO HUU KATIKATI KULIA GEOFREY NYANG'ORO KATIKATI AKIMKABIDHI FEDHA ZA MSAADA FRANK KIWELE (21) FEDHA HIZO ZIMETOLEWA NA WASOMJA WA GAZETI LA MWANANCHI NA MCHANGO HUU NI KWAAJILI YA KUCHANGIA GHARAMA ZA MATIBABU YA TATIZO LINALOMSUMBUA TANGU KUZALIWA KWAKEWANAOSHUHUDI TUKIO HILO KUSHOTO NA AFISA USTAWI WA JAMII MKUU WA MANISPAA YA IRINGA GASPER NSANYE NA KULIA NI MJOMBO WA KIJANA HUYO THOMAS NGANDANGOHABARI
|
Thursday, June 12, 2014
FRANK KIWELE AWASHUKURU WALIOMCHANGIA
Sunday, May 25, 2014
Kiwele:NAHITAJI SH 3.6 MILIONI KUPATA TIBA YA TATIZO LINALONISIBU
MAKALA
Kwa kifupi kiwele anasumbuliwa na tatizo la viongu vinavyotumika kuzuia haja ndogo na kubwa kutoka kushindwa kufanya kazi.
Binafsi ninatoa shukurani zangu za dhati kwa wale waliofanikiwa kuyasoma makala ya Frenk Kiwele (21)katika gazeti la Mwananchi Mwananchi Jumapili toleo la Mei 3 mwaka huu.
Wengi wamehamsika na kuanza kumchangia mungua awabariki sana na awazidishie pale palipopungua ombi langu naomba muendelea kumchangii ili pamoja tuweze kumrejeshea kijana huyu matumaini ya kufurahia maisha yake hapa duniani.
Ukikutana naye mitaani ama nyumbani kwake akiwa amepumzika
na hata kama utamkuta akifanya baadhi ya shughuli kwa lengo la kujipatia kipato
kamwe huwezi kuadhani kama kijana huyo Frank Kiwele (21) anatatizo lolote.
Nikijana mtulivu na mwenye sura ya ucheshi mda wote
utakapokuwa amekaa naye na hata kuzungumza na,ni vigumu kuamini kama
anakabiriwa na tattizo la kutwa na haja kubw ana ndogo tatizo lililodumu tangu kuzaliwa kwake hadi
sasa.
“Tatizo hili nimezaliwa nalo kwani katika sehemu ya kiuono
unapoanzia uti wa mgongo ninauvimbe,wataalamu wanasema ndio unaosababisha uwepo
wa tatizo hilo,kimsingi limenitesa sana limenitenga na jamii na marafiki
kutokana na kutokwa na haja ndogo na kubwa bila mufulililozo bila ya hata kujitambua.”anasema
Kiwele.
Kiwele ni mtoto wa pili katika familia ya Eliuta Kiwele
ambaye amefariki duniani miaka 7 (mwaka 2007 akitanguliwa na mama mazazi wa
Frank ,Sarah Ngadango aliyefariki mwaka 2002.
Kwa kifupi kiwele anasumbuliwa na tatizo la viongu vinavyotumika kuzuia haja ndogo na kubwa kutoka kushindwa kufanya kazi.
Binafsi ninatoa shukurani zangu za dhati kwa wale waliofanikiwa kuyasoma makala ya Frenk Kiwele (21)katika gazeti la Mwananchi Mwananchi Jumapili toleo la Mei 3 mwaka huu.
Wengi wamehamsika na kuanza kumchangia mungua awabariki sana na awazidishie pale palipopungua ombi langu naomba muendelea kumchangii ili pamoja tuweze kumrejeshea kijana huyu matumaini ya kufurahia maisha yake hapa duniani.
CHAI BORA MUFINDI INAVYONOGESHA KOMBE LA "MUUNGANO MUFINDI CUP"
Mwakilishi wa timu ya Zamalek ya Njombe kulia Shukuru Millinga akionyesha moja ya jezi alizokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Uzalishaji cha Kampuni ya Chai Bora ya Mufindi Mkoani Iringa Petronilla Alphone kushoto kwenye wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Kiwanda cha Chai bora Mjini Mafinga Wilayani Mufindi mkoani Iringa,katikati ni mratibu wa michuoano hiyo Daud Yasini
Viongozi wa kiwanda cha Chai bora,chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Mufindi,waratibu kombe la Muungano na wawakilishi wa timu washiriki wa kombe la muungano wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo iliyofanyika kwenye viwanja vya kiwanda hicho mjini Mafinga mkoani Iringa,waliosimama ni wawakilishi watimu washiriki.
HABARi
MWISHO
Viongozi wa kiwanda cha Chai bora,chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Mufindi,waratibu kombe la Muungano na wawakilishi wa timu washiriki wa kombe la muungano wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo iliyofanyika kwenye viwanja vya kiwanda hicho mjini Mafinga mkoani Iringa,waliosimama ni wawakilishi watimu washiriki.
HABARi
KOMBE la Muungano “Muungano Cup”
ambalo limeanza kutimua vumbi katika Viwanja vya Igowole na kile cha Wambi katika Wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa limepigwa jeki na kampuni ya Chai Bora, kwa
kupatiwa msaada wa jezi seti 6 pamoja na mipira 10 kwa ajili ya kuboresha
mashindano hayo.
Akikabidhi
jezi na mipira hiyo kwa
mratibu wa mashindano hayo ya kombe la Muungano- Daud Yasin, mkuu wa
idara ya uzalishaji wa Kampuni ya Chai Bora Petronilla Alphonce,
alisema lengo la msaada huo ni
kuyafanya mashindano hayo kuwa na muonekano wa pekee, shughuli
iliyofanyika
katika uwanja wa Chai Bora mjini Mafinga,.
Petronida amesema vijana hao
wanapaswa kujituma katika michezo ili kuonyesha vipaji na uwezo nyanda za
juu kusini, ikiwa pamoja na kutotumia vinywaji vyenye kileo ili kuwafanya wawe
na nguvu imara.
Aidha amesema misaada hiyo
imegharimu jumla ya shilingi Milioni 7.7 na kuwa kampuni kwa kutambua
hilo imetoa msaada huo kwa wachezaji wote, na mchango huo ni katika kuunga
mkono mashindano hayo kwa kuiwakirisha kampuni kwa kiwango cha hali ya juu.
“Kampuni kwa kuthamini michezo imeona
ni vema itoe jezi seti 6 na Mipira kumi, vifaa vyenye thamani ya shilingi
Milioni 7.7, mchango huu tulioutoa tunajua una manufaa na utatuletea ushindani
mkubwa”alisema Petronilla
Akipokea msaada huo mratibu wa
mashindano hayo ya Kombe la Muungano Daud Yasin alisema kampuni ya Chai imekuwa kiyadhamini mashindano
hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 1998.
Amewataka wachezaji kuthamini vifaa
hivyo kwa ubora wake kwani vina ubora wa hali ya juu, na kuwa matumaini yake ni
vilabu shiriki kufanya vyema ili kuitangaza kampuni hiyo kupitia michuano hiyo
inayozishirikisha timu za mikoa ya nyanda za juu kusini.
Alisema mashindano hayo ambayo yamezinduliwa Mei 24
katika uwanja wa shule ya msingi Igowole ambapo mashindano hayo yataendeshwa
katika viwanja viwili, kwa maana ya kiwanja cha wambi cha mjini Mafinga
na kiwanja Igowole shule ya msingi,
Uwanja wa Igowole utachezewa na timu
ya Mbeya city ya jijini Mbeya, Zamalek na timu ya Igowole
sekondari, huku mjini Mafinga katika uwanja wa Wambi kutakuwa
na mechi ya timu ya Benk ya wananchi Mucoba, timu ya chuo cha Incoment na timu
ya Black Cheeter ya mjini Iringa.
Amesema timu ya Mbaspo ambayo ni
mabingwa watetezi waliochukua kombe la Muungano mwaka 2013 wamepewa fulsa ya
kuingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali, ambapo amewataka wapenzi wa
soka na mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia vipaji vya vijana wa nyanda za
juu kusini.
Hata hivyo alisema mashindano hayo yamekuwa
na msisimko kwa kuwa yanahusisha vijana walio na umri chini ya miaka 20, huku
akiwataka wapenzi na mashabiki wa nyanda za juu kusini, kujitokeza kwa wingi
kutazama vipaji vya vijana wa nyanda za juu kusini.
Daud Yasini alisema kwa mwaka huu
niwa mwisho kwake kuratibu mashindano ya kombe la Muungano kwani
anastaafu na kuwa bingwa atachukua Kombe hilo moja kwa moja, kama ni kumbukumbu
kwa timu ya uratibu wake wa mashindano hayo.
Yasini alisema mashindano hayo yatakamilika Juni 11 mwaka
huu ambapo fainali ya kombe hilo mchezo wake utakachezwa katika uwanja wa Wambi
wa mjini Mafinga.
MICHUANO KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI
Mkuu wa kitengo cha uzalishaji wa kampuni ya Chai bora ya Mufindi makoani Iringa Petronilla Alphoce akipena mkono na
Lambardo Mvanda, mwakirishi wa timu ya Black Cheeter ya Iringa mjini wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msada wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Sh 7.7 milioni,Katikati mratibu wa mashindano hayo Daud Yasini
Saturday, May 24, 2014
Lumiye: Tumeanzisha chama kupinga manyanyaso
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) Ally Lumiye akizunguzunguza na wafugaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha mtakuja wilayani chunya jijini mbeya
HABARI
WAFUGAJI kote nchini wameshauriwa kujiunga na Chama cha
wafugaji Tanzania (CCWT) ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwamo vitendo vya unyanyasaji walivyodai wamekuwa wakitendewa
na baadhi ya viongozi na watendahi serikalini.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti
wa (CCWT) Taifa Ally Lumiye alipokuwa akizungumza na wafugaji kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mtakuja wilayani Chunya Jijini Mbeya .
Ally amesema kwa muda mrefu
jamii ya wafugaji imekuwa ikitendewa vitendo vya kinyama ikiwamo kuhamishwa
katika maeneo yao bila ya kufuata taratibu na wakati mwingine mifugo kukamatwa
huku wafugaji wakitozwa ushuru mkubwa kitendo kinachochangia kuwafilisi.
Amesema ndani ya chama hicho
wafugaji watapata fursa ya kutetewa pindi wanapofanyiwa vitendo vya uonevu
kwakuwa kimeajiri wanasheria kwa ajili ya kazi hiyo.
“Chama chetu kimepata usajil Desemba
mwaka jana,kama mnavyofahamu jamii ya wafugaji imekuwa kitendewa vitendo vya
unyanyasaji ,wafugaji kuhamishwa bila kufuata utaratibu,mifugo kukamatwa na
kuzwa faini kubwa na hata wakati mwingine kutaifishwa…sasa wafugaji mmepata
mtetezi wenu mtumieni”alisema Lumiye na kuongeza kuongeza:
“Kwa
sasa chama chetu kimeajili wanasheria ambao jukumu lao ni kukusanya taarifa
mbalimbali kutoka kwa wafugaji ili kuona kama kunawafugaji wametendewa vitendo
vya ukiukwaji wa sheria hatua ziweze kuchukuliwa dhida ya wahusika”alisema.
Subscribe to:
Comments (Atom)




