Mwakilishi wa timu ya Zamalek ya Njombe kulia Shukuru Millinga akionyesha moja ya jezi alizokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Uzalishaji cha Kampuni ya Chai Bora ya Mufindi Mkoani Iringa Petronilla Alphone kushoto kwenye wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Kiwanda cha Chai bora Mjini Mafinga Wilayani Mufindi mkoani Iringa,katikati ni mratibu wa michuoano hiyo Daud Yasini
Viongozi wa kiwanda cha Chai bora,chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Mufindi,waratibu kombe la Muungano na wawakilishi wa timu washiriki wa kombe la muungano wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo iliyofanyika kwenye viwanja vya kiwanda hicho mjini Mafinga mkoani Iringa,waliosimama ni wawakilishi watimu washiriki.
HABARi
MWISHO
Viongozi wa kiwanda cha Chai bora,chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Mufindi,waratibu kombe la Muungano na wawakilishi wa timu washiriki wa kombe la muungano wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo iliyofanyika kwenye viwanja vya kiwanda hicho mjini Mafinga mkoani Iringa,waliosimama ni wawakilishi watimu washiriki.
HABARi
KOMBE la Muungano “Muungano Cup”
ambalo limeanza kutimua vumbi katika Viwanja vya Igowole na kile cha Wambi katika Wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa limepigwa jeki na kampuni ya Chai Bora, kwa
kupatiwa msaada wa jezi seti 6 pamoja na mipira 10 kwa ajili ya kuboresha
mashindano hayo.
Akikabidhi
jezi na mipira hiyo kwa
mratibu wa mashindano hayo ya kombe la Muungano- Daud Yasin, mkuu wa
idara ya uzalishaji wa Kampuni ya Chai Bora Petronilla Alphonce,
alisema lengo la msaada huo ni
kuyafanya mashindano hayo kuwa na muonekano wa pekee, shughuli
iliyofanyika
katika uwanja wa Chai Bora mjini Mafinga,.
Petronida amesema vijana hao
wanapaswa kujituma katika michezo ili kuonyesha vipaji na uwezo nyanda za
juu kusini, ikiwa pamoja na kutotumia vinywaji vyenye kileo ili kuwafanya wawe
na nguvu imara.
Aidha amesema misaada hiyo
imegharimu jumla ya shilingi Milioni 7.7 na kuwa kampuni kwa kutambua
hilo imetoa msaada huo kwa wachezaji wote, na mchango huo ni katika kuunga
mkono mashindano hayo kwa kuiwakirisha kampuni kwa kiwango cha hali ya juu.
“Kampuni kwa kuthamini michezo imeona
ni vema itoe jezi seti 6 na Mipira kumi, vifaa vyenye thamani ya shilingi
Milioni 7.7, mchango huu tulioutoa tunajua una manufaa na utatuletea ushindani
mkubwa”alisema Petronilla
Akipokea msaada huo mratibu wa
mashindano hayo ya Kombe la Muungano Daud Yasin alisema kampuni ya Chai imekuwa kiyadhamini mashindano
hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 1998.
Amewataka wachezaji kuthamini vifaa
hivyo kwa ubora wake kwani vina ubora wa hali ya juu, na kuwa matumaini yake ni
vilabu shiriki kufanya vyema ili kuitangaza kampuni hiyo kupitia michuano hiyo
inayozishirikisha timu za mikoa ya nyanda za juu kusini.
Alisema mashindano hayo ambayo yamezinduliwa Mei 24
katika uwanja wa shule ya msingi Igowole ambapo mashindano hayo yataendeshwa
katika viwanja viwili, kwa maana ya kiwanja cha wambi cha mjini Mafinga
na kiwanja Igowole shule ya msingi,
Uwanja wa Igowole utachezewa na timu
ya Mbeya city ya jijini Mbeya, Zamalek na timu ya Igowole
sekondari, huku mjini Mafinga katika uwanja wa Wambi kutakuwa
na mechi ya timu ya Benk ya wananchi Mucoba, timu ya chuo cha Incoment na timu
ya Black Cheeter ya mjini Iringa.
Amesema timu ya Mbaspo ambayo ni
mabingwa watetezi waliochukua kombe la Muungano mwaka 2013 wamepewa fulsa ya
kuingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali, ambapo amewataka wapenzi wa
soka na mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia vipaji vya vijana wa nyanda za
juu kusini.
Hata hivyo alisema mashindano hayo yamekuwa
na msisimko kwa kuwa yanahusisha vijana walio na umri chini ya miaka 20, huku
akiwataka wapenzi na mashabiki wa nyanda za juu kusini, kujitokeza kwa wingi
kutazama vipaji vya vijana wa nyanda za juu kusini.
Daud Yasini alisema kwa mwaka huu
niwa mwisho kwake kuratibu mashindano ya kombe la Muungano kwani
anastaafu na kuwa bingwa atachukua Kombe hilo moja kwa moja, kama ni kumbukumbu
kwa timu ya uratibu wake wa mashindano hayo.
Yasini alisema mashindano hayo yatakamilika Juni 11 mwaka
huu ambapo fainali ya kombe hilo mchezo wake utakachezwa katika uwanja wa Wambi
wa mjini Mafinga.


No comments:
Post a Comment