Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania MAT Dk Namala Mkopi akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari
HUENDA huduma za tiba katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili MNH,Taasisi ya Mifupa MOI na maeneo mbalimbali nchini zikazorota kuanzia machi 7 mwaka huu baada ya madaktari kutangaza mgomo kiaina.
Madaktari hao kupitia kwa uongozi wao wa Chama cha Madaktari Tanzania MAT na Jumuiya ya Madaktari iliyoundwa kufanya kazi ya kusimamia madai yao wamebandika matangazo katika maeneo mbalimbali ya MNH na MOI yanayodai huduma zingesitisha kesho ikiwa Waziri na Naibu wake hawajajiuzulu.
“Kama tulivyotaarifiana kwenye kikao cha Machi 3 mwaka huu,makubaliano yaliyofikwa katika kikao cha 2/3 baina yetu na serikali ni kuwa,ili meza ya mazungumzo iweze kuendelea ni lazima waziri na Naibu wake wawe wamejiuzulu au kuwajibishwa”anasema sehemu ya tangazo lililosainiwa na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania MAT DK Namala Mkopi.
Dk Mkopi alitetea uamuzi wa kutandaza matangazo hayo kuwa ni jambo zuri la kuwajenga watu wanaoendelea kupata huduma katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili MNH na Taaisi ya Mifupa MOI kisaikolojia juu ya kinachoendelea na kuwawezesha kuchukua hatua pale inapobidi.
Alisema hatua hiyo ya kutaarifa umma inaweza kutafisiliwa (Negative) hasi au (postive) chanya lakini akasisitiza hilo la kuwajulisha watu linaweza kuwasaidia kufanya uamuzi iwe kuahamisha ndugu zao kupeleka katika hosptali za binafsi au vinginevyo
Akieleza sababu za kumtaka Waziri na Naibu wake kujiuzulu au kuwajibishwa anasema:
“Yapo mambo mengi sana yanafanywa kinyume na utaratibu na yote hayo ni sababu ya kukosekana kwa uongozi bora,imefikia hatua dawa za kutibia wagonjwa hakuna,vifaa vya kufanyia kazi Hospitali inakosa gase ya Oxgen na watu wanapoteza maisha kutokana na hilo”anasema Dk Mkopi.
Alisema suala la pili tuhuma zote zilizoelekezwa Wizara katika Wizara ya Afya zimetendeka wakati Waziri Mponda na Naibu wake wakiwa kwenye nafasi zao.
"Huwezi sema eti haya hayajui nani asiyefahamu majibu ya kejeli waliyotoa Waziri na Naibu wake kwa madaktari walipofuatilia madai yao?:ndiyo sababu tunasema tunachokwenda kujadili tunataka kiufanye mgomo kuwa historia itakuwaje watekelezaji wake wawe walioshindwa kushughulikia uovu"anasema.
Kuhusu hali ya huduma kuwa mbaya na athari zake Dk Mkopi ambaye ni Daktari bingwa wa watoto alitolea mfano wa mgonjwa aliyekuwa akimuhudumia kuwa alipoteza maisha kwa kukosa sukari ambayo kama angepatiwa maisha yake yangeokolewa.
"Huwezi sema eti haya hayajui nani asiyefahamu majibu ya kejeli waliyotoa Waziri na Naibu wake kwa madaktari walipofuatilia madai yao?:ndiyo sababu tunasema tunachokwenda kujadili tunataka kiufanye mgomo kuwa historia itakuwaje watekelezaji wake wawe walioshindwa kushughulikia uovu"anasema.
Kuhusu hali ya huduma kuwa mbaya na athari zake Dk Mkopi ambaye ni Daktari bingwa wa watoto alitolea mfano wa mgonjwa aliyekuwa akimuhudumia kuwa alipoteza maisha kwa kukosa sukari ambayo kama angepatiwa maisha yake yangeokolewa.
“Nilihangaika sana kutafuta Glucous kikawaida mtu anatakiwa kuwa na 3 hadi 5 lakini mtoto yule alikuja na 0.1,ninasema haya kwa uchungu ili mjue madaktari tunavyohangaika na tunamambo mengi hatusemi”anasema na kuongeza:
“Baada ya kukosa huduma hiyo huku mtoto akiwa hoi nilikwenda wodi A,B,Makuti kote kulikuw ahakuna ndipo nilipokwenda kule wanakolazwa watoto mahututi huku nilipata glucous nayo ilikuwa imeshatumika,nilikuja kumpa mtoto na akapata fahamu lakini alipotez amisha”anasema.
Dk Mkopi anafafanua kuwa hatua ya kutaka uongozi mawaziri kuiondoka kwenye nyazifa zao ni kutokana na namna wao walivyoshindw akushughukilia tatizo la Madaktari tangu mwanzo hadi walipoingia kwenye mgomo.
Alisema ili kuhakikisha majadiliano ya sasa yanafuta tatizo la mgomo hadi watakapostaafu na kulifanya migomo ya Madaktari kuwa historia ni lazima kuwapo kwa viongozi wa kisiasa ambao ndio wasimamizi wa makubaliano hayo na ni Waziri na Naibu wake.
“Hebu fikiri itakuwaje waziri aliyetoa majibu ya kejeli kiasi kile aliyewadharau Madaktari leo ndiye aje kusimamia makubaliano baina yao na serikali kutakuwa na usimamizi wenye ufanisi wa kina?hata Madaktari hawatakuwa na furaha katika utendaji wao wakifanya kazi chini ya Waziri na Naibu wake huyo”anasema.


No comments:
Post a Comment