Baadhi ya ndugu wakihudumia mgonjwa wao katika moja ya wodi zilizopo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili wakati wa mgomo wa madaktari
SAKATA LA MGOMO
MADHARA yameanza kujitokeza kufautia mgomo wa Madaktari ambao umeingia siku ya pili leo hapa nchini na umeshika kasi zaidi katika Taaisis ya Mifupa (MOI) na Hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mgomo huu uneendelea tena nah ii ni kufautia tangazo lilitolewa juzi na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Namala Mkopi muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha fargha cha Madaktari.
“Tunasikitika kutoa taarifa hizi kwa umma kuwa sasa Madaktari wanarudi katika mgomo na utakuwa wa nchi nzima,wanawaomba wananchi kuelewa kuwa lengo lao ni kuboresha huduma za afya nchini,uzorotaji wa huduma ninyi nyote mnaufahamu na hata wakilazimishwa itakuwa ni kazi bure”anasema Mkopi.
Dk Mkopi aliwaomba wadau mbalimbali na pia waandishi wa habari kutopotosha nia yao huku akisisitiza wameshindw akuendelea na kikao cha majadiliano sababu wanasubiri utekelezwaji wa hatua ya kwanza ya makubaliano waliyotiliana saini na serikali ya kutaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Naibu wake kujiuzuru nyazifa zao.
Mgomo umeshika kasi Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupupa (MOI) kufuatia tamko la kikao cha Madaktari bingwa kilichomalizika juzi na kutoa masimamo wa kurejea katika mgomo huo nchi nzima.
Eneo lililoathiriwa zaidi na mgomo huo kwa leo ni MOI ambapo wagonjwa wote waliofika kupata huduma za vipimo mbalimbali katika Kiliniki, waliamuliwa kurudi nyumbani kwao hadi watakapopata taarifa za kumalizika kwa mgomo huo kupitia vyombo vya habbari
Baadhi ya wagionjwa walizungumzia hali hiyo kuwa ni hatari huku wakiitupia lawama serikali kwa kushindw kuchukua hatua sitahiki za kumaliza mgomo ili hali wao wanazidi kuteseka.
Kulwa Amiri (30) Mkazi wa jijini Dar es Salaa alimtaka Rais Jakaya Kikwete,Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mawaziri wanaokataliwa kutafakari hatua zaiidi ili kunusuru maisha yao na ya jamaa zao.
Alisema mgomo siyo tu unaathiri afya ya mgonjwa pekee bali unarudisha nyuma maendeleo ya mtu mmojamoja na familia kwa ujumla sababu unakwamisha shughuli za maendeleo za kila siku.
“Katika mgomo wanaoathirika ni wengi siyo tu mgonjwa,wapo waangalizi wa wagonjwa nao wanapoteza muda kwa kumsindikiza mgonjwa,nauli na pia hata kazi wanazozifanya zinasimama”alisema Amiri na kuhoji:
“Hivi ni kweli serikali haioni mateso tunayopata?,inashindwa nini kuwawajibishwa hao mawaziri hata kutaka kututoa sisi kafara?mbona Mh Edward Lowasa alipokuwa waziri Mkuu alijiuzuru,tunaomba nao mawaziri wanaokataliwa watafakari kwa makini kwani tunaoteseka ni sisi”alisema Amiri ambaye alivunjika Uti wa Mgongo.
Wakati mgonjwa huyo akilalamikia kitendo hicho,baadhi ya ndugu wa wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa Wodini walifika hosptalini hapo na kuanza kuahamisha wagonjwa wao.
Marwa Chacha na ndugu zake walimuhamisha Edina Kameta aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Mwaisela huku akieleza dhamira ya kufikia uamuzi huo kuwa imetokana na hali ya kutisha na isiyotabirika iliyopo katika hosptali hiyo.
“Tumeamua kumchukua bibi yetu Edina Kameta na kumhamishia katika hosptali ya binafsi ya Regency ya jijini hapa, sababu tumeona hali katika eneo hili inatisha,kwanza mambo yanaingiliana wapo wanaofahamu na wengine hawafahamu”alisema Marwa.
MOI yafunga huduma za OPD
Taasisi ya Mifupo MOI ilitangaza rasimi kufunga Kiliniki zinazotoa huduma kwa wagonjwa wan je (OPD) huku ikitaja sababu za kufanya hivyo ni kutokana na mgomo wa madaktari.
Msemaji wa Taaisi hiyo Juma Almasi aliwambia waandishi wa habari kuwa hatua hiyo imelenga kuwawezesha madaktari wachache waliopo kuhudumia idado ya wagonjwa 237 waliolazwa wodini.
“Taasisi inawagonjwa 237 waliolazwa wodini,na madaktari wanaoendelea kufanya kazi ni wakuu wa idara na wenye nafasi za uongozi ambao idadi yao haizidi 15”alisema Almas.
Alifafanua kuwa katia siku za kawaida huduma za Kiliniki kwa wagonjwa wanje hutolewa na zaidi ya Madaktari 20 huku idadi ya wagonjwa ikitofautiana kutokana na aina ya Kiliniki zilizopangwa kwa siku husika.
“MOI inamadaktari zaidi ya 70 na kila siku huduma za Kiliniki za nje hutolewa na Madaktari zadi ya 20,kutokana na mgomo huu tumeamua kusitisha huduma za wagonjwa nje wanaokuja kwa ajili ya Kiliniki na kwamba tutaendelea kuwahudumia walioko wodini.
Pia msemaji huyo alisema huduma nyingine zitakazopatikana katika Taaisi hiyo ni zinazotolewa na kitengo cha dhararu.
Tughe yatoa tamko
Ikiwa ni siku ya pili Tangu Mgomo kuanza Shirikisho la Vyama vya Wafanya kazi wa Serikali Kuu na Afya Tughe imetoa tamkoa la kuzitaka pande mbili zinazolumbana kutumia busara kumaliza mgomo huo.
Katibu Mkuu wa Tughe Taifa Ali Kiwenge anasema mgomo huo ni matokea ya pande hizo mbili kutegeana na kutoaminia katika kufikia mwafaka juu ya mchakato wa kumaliza tatizo.
“Sisi tunasema ,serikali na Madaktari,hayo yanayoendelea wananchi wanawashangaa,tunasema hivyo sababu wanajua madai ya Madaktari serikali iliyapokea na kuahidi kuyafanyia kazi na ndiyo sababu Waziri Mkuu Pinda aliunda tume,lakini nao madaktari wakakubali kutoa nafasi ya kusubili ili madai hayo yafanyiwe kazi”anasema Kiwenge.
Kiwenge anasema alisisituiza kuwa msimamo wa Tughe ni kuwa suluhu lazima ifikiwa kupitia kwenye vikao na kuonya kila upande kutumia busara kwa nia ya kunusuru maisha ya watanzania.
Kiwenge aliionya serikali kwa kutumia misema mbalimbali ambapo aliitaka isiwe na tabia kama za binadamu katika kushughulikia matatizo yaliyopo katika jamii.
“Sisi tunasema suluhu ya mgogoro lazima upatikane kupitia vikao,tatizo la mgogoro wa sasa baina ya Madaktari na serikali limetokana na kila upande kuwa na papara katika kushughuklikia madai hayo ni hii ni kama tabia ya mtu,tabia ya mwanadamu mara zote inapotokea tatizo husakizia mwenzake ili aonekana mwenye kosa,serikali ni chombo cha umma hivyo isingekuwa kama binadamu”alisema.
Kiwenge aliitaka serikali kufanya kazi kama chombo cha umma ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala mbalimbali kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni zilizopo.
Alisema ni jambo la kawaida kwa serikali nyingi hususani za kiafirika na Tanzania ikiwemo kufanya kazi kinyume na taratibu jambo ambalo husababisha manungĂșniko,mgogoro,migomo baridi na baadaye migomo kamili na maandamano.

No comments:
Post a Comment