Friday, March 9, 2012

RAIS KIWETE AJITOSA RASMI MGOMO WA MADAKTARI SASA AWAITA IKULU




Rais Jakaya Kikwete amekipeana mkono na mmoja wa wajumbe wa jumuiya ya Madaktari walifika Ikulu kuitikia wito wa Rais kikwete kujadili maandamano




Suluhu ya mgomo
HUKU maisha ya watanzania wagonjwa na wale wanaouguza ndugu zao wakiendelea kukata tamaa ya maisha kufuatia kukosa huduma zinazotokana na mgomo wa madaktari unaoingia siku  ya tatu leo,Rais Jakaya Kikwete amewaita madaktari hao Ikulu.
Hatua ya Rais Kikwete imekuja ikiwa ni siku moja tu tangua Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuahirisha ziara ya iliyokuwa aifanye kwa muda wa siku 10 Mkoani Mwanza lengo likiwa kushughulikia mgomo huo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa Nchi kujitosa katika mgogoro huo mkubwa kupata kutokea tangu uatwala wake wa awamu ya pili uingie madakrakani.
Awali alitangazwa kuwa Rais Kikwete alitaraji kuzungumza na Wananchi kupitia vyombo vya habari leo majira ya saa kumi jioni ambapo angehutubia wazee wa jiji la Dar es Salaam lakini ghafla suala hilo likaahirishwa na kisha kuamua kukutana na Madaktari.
Huenda mazungumzo yake na Madaktari yakaleta suruhu ya kudumu ya mgogoro ambao hadi sasa umesababisha athari na usumbufu kwa baabdhi ya watu ambao dnugu zao wamelazwa hospitalini.
Wakati Rais Kikwete akikutana na uongozi wa Madaktari hao hali katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),Taasisi ya Mifupa (MOI) na hosptali nyingine jijini Dar es Salaam huduma zilikuwa zimezorota.
Mgomo unafanyika wakati ambapo hivi karibuni Rais Kikwete aliwapa pole umma wa watanzani kutokana na mgomo uliositishwa Februari 9 mwaka huu kufuatia kikao cha Maridhiano baina ya Madaktari na Waziri Mkuu na kudai kuwa serikali itahakikisha hilo halijirudii.

Thursday, March 8, 2012

MGOMO WA MADAKTARI WAANZA KUATHIRI WANYONGE



Baadhi ya ndugu wakihudumia mgonjwa wao katika moja ya wodi zilizopo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili wakati wa mgomo wa madaktari

SAKATA LA MGOMO
MADHARA yameanza kujitokeza kufautia mgomo wa  Madaktari ambao umeingia siku ya pili leo hapa nchini na umeshika kasi zaidi katika Taaisis ya Mifupa (MOI) na Hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mgomo huu uneendelea tena nah ii ni kufautia tangazo lilitolewa juzi na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Namala Mkopi muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha fargha cha Madaktari.
“Tunasikitika kutoa taarifa hizi kwa umma kuwa sasa Madaktari wanarudi katika mgomo na utakuwa wa nchi nzima,wanawaomba wananchi kuelewa kuwa lengo lao ni kuboresha huduma za afya nchini,uzorotaji wa huduma ninyi nyote mnaufahamu na hata wakilazimishwa itakuwa ni kazi bure”anasema Mkopi.
Dk Mkopi aliwaomba wadau mbalimbali na pia waandishi wa habari kutopotosha nia yao huku akisisitiza wameshindw akuendelea na kikao cha majadiliano sababu wanasubiri utekelezwaji wa hatua ya kwanza ya makubaliano waliyotiliana saini na serikali ya kutaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Naibu wake kujiuzuru nyazifa zao.

Mgomo umeshika kasi Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupupa (MOI) kufuatia tamko la kikao cha Madaktari bingwa kilichomalizika juzi na kutoa masimamo wa kurejea katika mgomo huo nchi nzima.
Eneo lililoathiriwa zaidi na mgomo huo kwa leo ni   MOI ambapo wagonjwa wote waliofika kupata huduma za vipimo mbalimbali katika Kiliniki, waliamuliwa kurudi nyumbani kwao hadi watakapopata taarifa za kumalizika kwa mgomo huo kupitia vyombo vya habbari
Baadhi ya wagionjwa walizungumzia hali hiyo kuwa ni hatari huku wakiitupia lawama serikali kwa kushindw kuchukua hatua sitahiki za kumaliza mgomo ili hali wao wanazidi kuteseka.
 Kulwa Amiri (30) Mkazi wa jijini Dar es Salaa alimtaka  Rais Jakaya Kikwete,Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mawaziri wanaokataliwa kutafakari hatua zaiidi ili kunusuru maisha yao na ya jamaa zao.

Alisema mgomo siyo tu unaathiri afya ya mgonjwa pekee bali unarudisha nyuma maendeleo ya mtu mmojamoja na familia kwa ujumla sababu unakwamisha shughuli za maendeleo za kila siku.

“Katika mgomo wanaoathirika ni wengi siyo tu mgonjwa,wapo waangalizi wa wagonjwa nao wanapoteza muda kwa kumsindikiza mgonjwa,nauli na pia hata kazi wanazozifanya zinasimama”alisema Amiri na kuhoji:
“Hivi ni kweli serikali haioni mateso tunayopata?,inashindwa nini kuwawajibishwa hao mawaziri   hata kutaka kututoa  sisi kafara?mbona Mh Edward Lowasa alipokuwa waziri Mkuu alijiuzuru,tunaomba nao mawaziri wanaokataliwa watafakari kwa makini kwani tunaoteseka ni sisi”alisema Amiri ambaye alivunjika  Uti wa Mgongo.
Wakati mgonjwa huyo akilalamikia kitendo hicho,baadhi ya ndugu wa wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa Wodini walifika hosptalini hapo na kuanza kuahamisha wagonjwa wao.
Marwa Chacha na ndugu zake walimuhamisha Edina Kameta aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Mwaisela huku akieleza dhamira ya kufikia uamuzi huo kuwa imetokana na hali ya kutisha na isiyotabirika iliyopo katika hosptali hiyo.
“Tumeamua kumchukua bibi yetu Edina Kameta na kumhamishia katika hosptali ya binafsi ya Regency ya jijini hapa, sababu tumeona hali katika eneo hili inatisha,kwanza mambo yanaingiliana wapo wanaofahamu na wengine hawafahamu”alisema Marwa.
MOI yafunga huduma za OPD
Taasisi ya Mifupo MOI ilitangaza rasimi kufunga Kiliniki zinazotoa huduma kwa wagonjwa wan je (OPD) huku ikitaja sababu za kufanya hivyo ni kutokana na mgomo wa madaktari.
Msemaji wa Taaisi hiyo Juma Almasi aliwambia waandishi wa habari kuwa hatua hiyo imelenga kuwawezesha madaktari wachache waliopo kuhudumia idado ya wagonjwa 237 waliolazwa wodini.
“Taasisi inawagonjwa 237 waliolazwa wodini,na madaktari wanaoendelea kufanya kazi ni wakuu wa idara na wenye nafasi za uongozi ambao idadi yao haizidi 15”alisema Almas.
Alifafanua kuwa katia siku za kawaida huduma za Kiliniki kwa wagonjwa wanje hutolewa na zaidi ya Madaktari 20 huku idadi ya wagonjwa ikitofautiana kutokana  na aina ya Kiliniki zilizopangwa kwa siku husika.
“MOI inamadaktari zaidi ya 70 na kila siku huduma za Kiliniki za nje hutolewa na Madaktari zadi ya 20,kutokana na mgomo huu tumeamua kusitisha huduma za wagonjwa nje wanaokuja kwa ajili ya Kiliniki na kwamba tutaendelea kuwahudumia walioko wodini.
Pia msemaji huyo alisema huduma nyingine zitakazopatikana katika Taaisi hiyo ni zinazotolewa na kitengo cha dhararu.


Tughe yatoa tamko
Ikiwa ni siku ya pili Tangu Mgomo kuanza Shirikisho la Vyama vya Wafanya kazi wa Serikali Kuu na Afya Tughe imetoa tamkoa la kuzitaka pande mbili zinazolumbana kutumia busara kumaliza mgomo huo.
Katibu Mkuu wa Tughe Taifa Ali Kiwenge anasema  mgomo huo ni matokea ya pande hizo mbili kutegeana na kutoaminia katika kufikia mwafaka juu ya mchakato wa kumaliza tatizo.
“Sisi tunasema ,serikali na Madaktari,hayo yanayoendelea wananchi wanawashangaa,tunasema hivyo sababu wanajua madai ya Madaktari serikali iliyapokea na kuahidi kuyafanyia kazi na ndiyo sababu Waziri Mkuu Pinda aliunda tume,lakini nao madaktari wakakubali kutoa nafasi ya kusubili ili madai hayo yafanyiwe kazi”anasema  Kiwenge.
Kiwenge anasema alisisituiza kuwa msimamo wa Tughe ni  kuwa suluhu lazima ifikiwa kupitia  kwenye vikao na kuonya kila upande kutumia busara kwa nia ya kunusuru maisha ya watanzania.
Kiwenge aliionya serikali kwa kutumia misema mbalimbali ambapo aliitaka isiwe na tabia kama za binadamu katika kushughulikia matatizo yaliyopo katika jamii.
“Sisi tunasema suluhu ya mgogoro lazima upatikane kupitia vikao,tatizo la mgogoro wa sasa  baina ya Madaktari na serikali limetokana na kila upande kuwa na papara katika kushughuklikia madai hayo ni hii ni kama tabia ya mtu,tabia ya mwanadamu mara zote  inapotokea tatizo husakizia  mwenzake ili aonekana mwenye kosa,serikali ni chombo cha umma hivyo isingekuwa kama binadamu”alisema.
Kiwenge  aliitaka serikali kufanya kazi kama chombo cha umma ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala mbalimbali kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni zilizopo.
Alisema ni jambo la kawaida kwa serikali nyingi hususani za kiafirika na Tanzania ikiwemo kufanya kazi kinyume na taratibu jambo ambalo husababisha manungĂșniko,mgogoro,migomo baridi na baadaye migomo kamili na maandamano.

Tuesday, March 6, 2012

MGOMO WA MADAKTARI WATANGAZWA KIAINA DAR


 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madktari Dk Stephen Ulimboka akitoa msimamo wa Madaktari kuhusu madai yao dhidi ya serikali,kushoto ni katibu wa Jumuiya hiyo  Dk Edwin Chitega na kulia ni Mjumbe wa Jumiya Dk Rahm Hingosa.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania MAT Dk Namala Mkopi akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari
HUENDA huduma za tiba katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili MNH,Taasisi ya Mifupa MOI  na maeneo mbalimbali nchini zikazorota kuanzia machi 7 mwaka huu baada ya madaktari kutangaza mgomo kiaina.
Madaktari hao kupitia kwa uongozi wao wa Chama cha Madaktari Tanzania MAT na Jumuiya ya Madaktari iliyoundwa kufanya kazi ya kusimamia madai yao wamebandika matangazo  katika maeneo mbalimbali ya MNH na MOI yanayodai huduma zingesitisha kesho ikiwa Waziri na Naibu wake  hawajajiuzulu.
“Kama tulivyotaarifiana kwenye kikao cha Machi 3 mwaka huu,makubaliano yaliyofikwa katika kikao cha 2/3 baina yetu na serikali ni kuwa,ili meza ya mazungumzo iweze kuendelea ni lazima waziri na Naibu wake wawe wamejiuzulu au kuwajibishwa”anasema sehemu ya tangazo lililosainiwa na Rais  wa Chama cha Madaktari Tanzania MAT DK Namala Mkopi.
Dk Mkopi alitetea uamuzi wa kutandaza matangazo hayo kuwa ni jambo zuri la kuwajenga watu wanaoendelea kupata huduma katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili MNH na Taaisi ya Mifupa MOI kisaikolojia juu ya kinachoendelea na kuwawezesha kuchukua hatua pale inapobidi.
Alisema hatua hiyo ya kutaarifa umma inaweza kutafisiliwa (Negative) hasi  au (postive) chanya lakini akasisitiza hilo la kuwajulisha watu linaweza kuwasaidia kufanya uamuzi iwe kuahamisha ndugu zao kupeleka katika hosptali za binafsi au vinginevyo
Akieleza sababu za kumtaka Waziri na Naibu wake kujiuzulu au kuwajibishwa anasema:
“Yapo mambo mengi sana yanafanywa kinyume na utaratibu na yote hayo ni sababu ya kukosekana kwa uongozi bora,imefikia hatua dawa za kutibia wagonjwa hakuna,vifaa vya kufanyia kazi  Hospitali inakosa gase ya Oxgen na watu wanapoteza maisha kutokana na hilo”anasema Dk Mkopi.
Alisema suala la pili tuhuma zote zilizoelekezwa Wizara katika Wizara ya Afya zimetendeka wakati Waziri Mponda na Naibu wake wakiwa kwenye nafasi zao.

"Huwezi sema eti haya hayajui nani asiyefahamu majibu ya kejeli waliyotoa Waziri na Naibu wake kwa madaktari walipofuatilia madai yao?:ndiyo sababu tunasema tunachokwenda kujadili tunataka kiufanye mgomo kuwa historia itakuwaje watekelezaji wake wawe walioshindwa kushughulikia uovu"anasema.

Kuhusu hali ya huduma kuwa mbaya na athari zake  Dk Mkopi ambaye ni Daktari bingwa wa watoto alitolea mfano wa mgonjwa aliyekuwa akimuhudumia kuwa alipoteza maisha kwa kukosa sukari ambayo kama angepatiwa maisha yake yangeokolewa.
“Nilihangaika sana kutafuta Glucous  kikawaida mtu anatakiwa kuwa na 3 hadi 5 lakini mtoto yule alikuja na 0.1,ninasema haya kwa uchungu ili mjue madaktari tunavyohangaika na tunamambo mengi hatusemi”anasema na kuongeza:
“Baada ya  kukosa huduma hiyo huku mtoto akiwa hoi nilikwenda wodi A,B,Makuti  kote kulikuw ahakuna ndipo nilipokwenda kule wanakolazwa watoto mahututi huku nilipata glucous nayo ilikuwa imeshatumika,nilikuja kumpa mtoto na akapata fahamu lakini alipotez amisha”anasema.
Dk Mkopi anafafanua kuwa hatua ya kutaka uongozi  mawaziri kuiondoka kwenye nyazifa zao ni kutokana na namna wao walivyoshindw akushughukilia tatizo la Madaktari tangu mwanzo hadi walipoingia kwenye mgomo.
Alisema ili kuhakikisha majadiliano ya sasa yanafuta tatizo la mgomo hadi watakapostaafu na kulifanya migomo ya Madaktari kuwa historia ni lazima kuwapo kwa viongozi wa kisiasa ambao ndio wasimamizi wa makubaliano hayo na ni  Waziri na Naibu wake.
“Hebu fikiri itakuwaje waziri aliyetoa majibu ya kejeli kiasi kile aliyewadharau Madaktari leo ndiye aje kusimamia makubaliano baina yao na serikali kutakuwa na usimamizi wenye ufanisi wa kina?hata Madaktari hawatakuwa na furaha katika utendaji wao wakifanya kazi chini ya Waziri na Naibu wake huyo”anasema.

Monday, March 5, 2012

MAWAZIRI WAJIFUNGIA OFISNI KUKWEPA WAANDISHI WA HABARI

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda kulia ni Naibu wake Dk Lucy Nkya

Kufuatia tishio la mgomo wa madaktari

WAKATI Madaktari wakitarajia kuanza mgomo kesho  wa kushinikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda na Naibu wake Dk Lucy Nkya kujiuzulu,mawaziri hao jana walijifungua ofisini kwao kutwa nzima wakikwepa kuzungumza na waandishi wa habari.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Madaktari walitoa tamko zito la  kuitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha vigogo hao wakisiasa kabla ya Jumatano wiki hii la la sivyo watagoma kufanya kazi.
 Madaktari wanawatuhumu kuwa viongozi hao ni chanzo cha mgomo uliotangazwa Januari 23 ambao ulisababisha vifo vya watu kadhaa na wenginewengi kuathirika kwa kile walichadai walishindwa kutimiza wajibu wao.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walifika katika ofisi za Maziri hao  mapema asubuhi wakita kujua msimamo wa vigogo hao wa kisiasa katika Wizara ya Afya juu ya tamko la Madaktari
Hata hivyo wanahabari haop kwa nyakati tofauti walikutana na wasaidizi wa mawaziri hao walidai vigogo hao hawako tayari kuzungumza na waandishi wa habari.
Katika Ofisi ya Waziri Mponda wanahabari walielezwa kuwa Waziri hayuko tayari kuzungumzia suala hilo kwa sababu liko juu ya uwezo wake.
“Nataka mfahamu kuwa waziri anajua uwepo wenu lakini hayuko tayari leo kuzungumza na waandishi wa habari,hawezi kuzungumzia suala hilo sababu lipom juu yab uwezo wake”alisema Mmoja wa maofisa katika ofisi ya Waziri Mponda.
Pia katika Ofisi ya Naibu waziri wa Wizara hiyo Dk Nkya waandishi walipoingia walikutana na mmoja wa wasaidizi ambaye alitoa kauli kama ya mtangulizi wake.
Baada ya waandishi kusubiri kwa muda mlefu,ilipofika saa saba mchana Ofisa katika Ofisi ya Waziri wa Afya ,aliwaeleza kuwa angerudi tena ofisini kumshauri Waziri Mponda atoke ili aweze kuzungumza na wandishi hao.
Lakini baada ya muda alitoka Msemaji wa Wizara hiyo aliyekuwa kwenye mkutabno wa wakurugenzi wa Idara zote za Wizara ya Afya Nsachris Mwamwaja  na kusisitiza kuwa mawaziri hawakuwa na cha kusema ju ya suala hilo sababu liko juu ya uwezo wao.
“Suala la madaktari linajadiliwa katika ngazi za juu,Mawaziri hawawezi kutoa maoni wala tamko lolote juu ya jambo hili”alisisitiza Mwamaja.


Mwamaja alisema suala hilo kwa sasa liko juu ya uwezo wa mawaziri hao na kusisitiza hawawezi kusema chochote huku akishauri waandishi kufuatilia ngazi za juu.
Msimamo wa Madaktari
Rais wa chama cha Madaktari Tanzania MAT Dk Namala Mkopi aliliambia Mwananchi kuwa msimamo wa madaktari upo palepale wa kutoendelea kufanya kazi endapo mawaziri hawatajiuzulu.
“Madaktari walishapitisha hili kwenye kikao chao,msimamo wao ni uleule kwamba wao hawataendelea kufanya kazi,ikiwa mawaziri hao watakuwa hawajajiuzulu ifikapo jumatano (kesho).

Wizarani
Wakati hali ikiwa hivyo,jana ukumbi wa mikuatno wa Wizara ya Afya ulitawaliwa na vikoa vya mda mrefu vilivyohusisha wakurugenzi wote wa idara za wizara ya Afya.
Habari za ndani zinasema wakurugenzi hao walikutana kujadili sakata hilo la madaktari na namna watakapokabiliana na tisho la mgomo huo mpya.
“Wakurugenzi wote wa Idara za Wizara wapo ndani ya kikao na wananendelea na mkutano chini ya Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk Dolnald Mbando,wanajadili suala la Madaktari,wanatafuta  namna watakavyokabiliana na tishio la mgomo huo mpya ”kilisema chanzo hicho.
Akizunguzia hilo Mwamaja alikiri kuwepo kwa kikao hicho lakini akabainisha kuwa kilikuwa cha uongozi wa Wizara na walikuwa wakijadili masuala mbalimbali na si kuhusu mgogoro wa madaktari.
“Nikweli kulikuwa na kikao hapa wizarani,hiki ni cha menejimenti walikutana kujadili mambo mbalimbali lakini hayahusiani na mgogorowa madaktari”alisema Mwamaja.
Kuhusu waziri na Naibu wake
Habari za ndani zinasema vigogo hao wateule wa rais hawana mpango wowote wa kujiuzulu.
Kwa mjibu wa mtoa habari hawana wasiwasi na tisho hilo sababu wanaamini madaktari hawatagoma bali wanatishio tu.
“Awali tulipata taarifa za wao kutaka kujiuzulu,lakini inasemekana kwa sasa hawana mpango huo na wanadai tamko la madaktari ni kutishia tu na wala hawawezi kugoma”kilisema chazno hicho.

SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI SEHEMU YA KWANZA

 Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari.Dk Stephen Ulimboka kabla ya kuanza kwa mkutano wa maridhiano ya kumaliza mgomo wa madaktari,Dk Ulimboka ni
                                   Waziri wa Afya na Usatawi wa Jamii Dk Hadji Mponda
ULIKUWA MGOMO WA KIHISTORIA
Wengi wanasema haijawahi tokea

JANUARI 23 mwaka huu  saa 11:30 jioni Dk Stephen Ulimboka mwenyekiti wa jumiya ya Madaktari akatangaza mgomo wa madaktari wenye lengo la kuishinikiza serikali kutekeleza madai yao.
Kutangazwa kwa mgomo kulikofanywa  na  jumuiya ya hiyo  kumekuja baada ya vikao vizito vilivyofanywa na madaktari hao  vikongozwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT)kushindwa kuzaa matanda.
Intenship chanzo cha mgogomo
Hilo haliwezi kukwepeka sababu chanzo cha mikutano ya madaktari ilitokana na hatua zilichukuliwa na serikali dhidi ya Madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili kutimuliwa katika vituo vyao vya kazi na kurejeshwa wizarani.
Madaktari hao ambao idadi kamili imekuwa ikishindw kujulikana kufuatia taarifa za awali kudai ni 225 huku habari toka wizarani zikidai ni 197 walitimuliwa na uongozi wa hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwakile kilichoelezwa ni kukiuka mkataba waliongia baina yao na uongozi wa hosptali hiyo.
Mmoja ya vipengele vya mkataba kinaeleza bayana kuwa ni marufuku kwa Interns kugoma wala kushawishi mgomo  kwa kipindi chote atakachokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.
Lakini wanataalam hao waligoma kwa muda wa siku mbili mfuliluzo kati ya  Januari 3 na 4 wakishinikiza serikali kuwalipa posho zao za miezi miwili zilizokuwa zimecheleweshwa.


Kwa muda wa simu mbili Mgomo uliotangazwa na Jumiya hiyo unadaiwa ni kutokana na hatua zilichukuliwa na lizochukuliwa madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili ambao walitimuliwa na uongozi wa Hosptali hiyo baada ya kuendesha mgomo wa siku mbili wakidai  posho zao za miezi miwili.
Idadi ya madaktari hao waliogoma Januari 2 mwaka huu ilikuwa na utata baada ya taarifa za awali zilitolewana uongozi wao kueleza kuwa walikuwa 225 huku tamko la serikali kupitia kwa Naibu waziri wa afya Dk Lucy Nkya ikisema ni 194.
Habari zuilieleza kuwa Madaktari hao walitimuliwa siku moja baada ya kulipw fedha zao ambapo uongozi walipowasili Hosptalini walikumbana na barua iliyowataka kuacha kazi na kurejea Wizarani.
Kufuatia hatua hiyo Junauri 12 mwaka huu  Chama cha Maktari Tanzania MAT kiliitisha mkutano wa dhararu wa baraza kuu na kujdali hoja kadhaa huku kikiipa serikali saa 72 kwa serikali kuwarejesha madaktari waliokuwa katika mafunzo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika tamko lao hilo Madaktari walielezea kuwa kufukuzwa kwa madaktari hao ni ukiukwaji wa haki za binadamu sababu wao walioshindw akuwalipa fedha zao ndio waliotenda kosa na hao ndio waliostahili adhabu
Baraza hilo la dhararua pia lilielezea dhamira ya kuendelea na mkutano wa Madaktari wote siku Juari 18 na kujadili mada mbalimbali ikiwamo ya hatima ya fya ya mtanzania na mazingira bora ya kazi
Majibu ya Wizara
Siku mbili baadaye,Januri 17 Wazira kupitia kwa Naibu waziri wa Afya  Dk Lucy Nkya ilitoa tamko lilipuuza madai ya madaktari hao huku likifafanua sababu za kuwatimua katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili kuwa ni kutokana na madaktari hao kuvunja mkataba na mwaajiri wao.
“Ieleweke kuwamba wataalamu hawa huingia mikataba na hosptali husika,mkataba wanaoingia umeainisha kwamba hawatagoma au kuanzisha mgomo”alisema Naibu waziri katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Dk Nkya alifafanua sababu za kuwatawanya katika vituo mbalimbali madaktari hao kuwa ilitokanana tathimini  iliyofanywa na wizara ambayo ilibaini kuwapo kwa idadi kubwa ya madaktari wa mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika mkutano huo pia Naibu waziri huyo alifafanua kuwa MAT ni miongoni mwa vyama vingine vya hiyari katika sekta ya Afya ambavyo kazi zake ni kufuatilia masuala ya wanachama wao kwa kutumia mifumo iliyowekwa  kisheria.
Dk Nkya alisema  wataalamu wote katika sekta ya afya katika husimamiwa na mabaraza ya Kitaaluma ambayo ni mamlaka  zilizoanzishwa kwa sheria za bunge.
Alisema mabaraza hayo ndiyo yenye dhamana kusimamia ufanisi wa mazoezi kwa vitendo na wahusika huku aitaka MAT kufanya kazi na Wizara iko tayari kushirikiana nao katika masuala yenye kuwezesha kuboresha huduma za afya.
Alionya na kukumbusha chama hicho kutekeleza majukumu yake kwa mjibhu wa katiba ya chama hicho kwa kushirikiana na serikali katika kuimarisha sekta ya afya na wataalamu walio kwenye sekta hiyo kwa manufaa ya nchi badala ya kujihusisha na harakati.
Tamko la Wizara  lawatibua  Madaktari
Katika mkutano wao wa Januri 18 mwaka huu Madakatari walisema majibu ya Wizara ya kudai madai yao hayana msingi ni ya kisiasa na yakuidhalisha taalamu yao.
Madaktari hao waliokutana katika ukumbi wa Rusian walikubaliana kutuma ujumbe wa watau watatu ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Chama hicho Dk Primus Saidia kwenda wizarani kumuita naibu huyo kwenye mkutano wao.
Hatua ya kumuita Naibu waziri huyo ililenga kupatikana kwa majibu ya maswali yao mengiambayo katika mkutano huo waliibua hoja nne na kuzijadili huku wakieleza kuwa suala la madaktari waliokuwa katikamafunzo ya vitendo lilikuwa linasubiri uamuzi baada ya serikali kushindwa kutekeleza madai yao  kwa muda uliokuwa umepangwa.
Ombi la kukutana na Naibu Waziri wa afya
Ujumbe toka Wizarani ulirejea na majibu kuwa Naibu huyo wawaziri alikuwa amekubaru kufika katika ukumbi wa mikutano wao lakini akaomba muda wa saa moja ili aweze kuwasilisna na wasaidizi wake.
Wakati Dk Saidia alikitoa taarifa hiyo,ghafla  alipoke simu na kutoka nje ya ukumbi na aliporejea aliwaeleza washiriki wa mkutano zaidi ya 200 waliokuwa wamejipanga kusikiliza naibu waziri huyo na kusema,
“Naibu waziri ameweataka radhi ninyi wote na kueleza kuwa hatakuja kwenye mkutanona badala yake tutakutana nae kesho saa nane mchana”alisema Saidia.
Chenga zikaanza
Siku ya pili ya mkutano Alhamisi ya Januari 19 Madaktari zaidi ya 300 walikusanyika mapema asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Don Bosco wakisubiri ujio wa Naibu waziri huyo wa Afya DK Lucy Nkya.
Wakati wao wakikusanyika ujumbe wa watu watatu ukiongozwa na Makamu wa Rais uliwasilisha barua pamoja na mihitasari ya vikao  na madai yao ya jumula na mahali wanapofanyia mkutano.
Wajumbe hao waliporudi walikuja na taarifa za Naibu waziri huyo kukataa kukutana na Madaktari katika ukumbi ulioandaliwa nao na badala yake wizara ingeandaa ukumbi  mwingine.
Madaktari walipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kilikuwa ni matumizi mabaya ya fedha sababu wao walikuwa tayari wamelipia ukumbi huo,lakini pia wakadai tukio hilo lingesababisha usumbufu kwao.
Wakiwa bado kwenye chumba hicho madaktari hao ghafla walielezwa tayari ukumbi ulikuwa umepatikana ambao ni Arnatoglo na kuwataka wao kwenda katika ukumbi huo kwa muda wa nusu saa vinginevyo Waziri huyo na ujumbe wake angeondoka.

Madaktari waligoma kwenda kwenye ukumbi huo kwa kile walichodai kuwa ni umbali wa kutoka eneo walipo na kwamba kutokana na hali ya usafiri ilivyokuwa muda wa nusu saa usingetosha kumkuta DK Nkya akiwa kwenye chumba cha mkutano.
Pia Dk Saidia alisema kundi la madaktari hao lingeonyesha taswira ya maandamano jambo ambalo lingesababisha usumbufu kwa wananchi wanaotumia njia hizo na pia kuhofia uwezekano wa Madaktari hao kukamatwa na Polisi kwa kisingizio cha kuandamana bila kibali.
Aidha madaktari hao wakasema Naibu waziri huyo ameonyesha dhararu kwa kitendo chake cha kwenda ukumbi mwingine ilihali akijua watu wako sehemu nyingine.

“Nirahisi kwa yeye kuja kuliko umati wa watu 300 kujaa barabarani kwa lengo la kumfuata,lakini kwanini ameenda Arnatouglo hali akijua watu wako huku,hii ni dhararu”alisema mmoja wa madaktari alipochangia kwenye mkutano wao.
Kufuatia mvutano huo Madaktari waligoma na kuweka azimoa la kukutana siku ya pili katika mwenndelezo wa mkutano wao huku wakiwa na wazo la kuona mamlaka nyingine za juu.

Kwa upande wake kutokana na mvutano huo Dk Nkya alikaririwa na vyombo vya habri akisema asingewasikiliza tena Madaktari na kuwataka madai yao yafikishwe serikalini kwa kutumia Shirikisho la vyama vya Serikali kuu na Afya (TUGHE) ambao wapo kisheria kushughulikia madai hayo.

"Madaktari hawa wameonyesha kiburi,kuanzia sasa sitawasikiliza na badala yake madai yao yote yawasilishwe wizarani kupitia Tughe na kama wataaendelea na vikao vyoa mfululizo kwa siku saba nitawafukuza"anasema Dk Nkya.


Harakati za kumona Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Siku iliyofuata Madaktari hao walikutana tena katika ukumbi wa mikutano wa Don Bosco na kudhamilia kumuona Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Madaktari huku wakiwa na imani kubwa na Waziri Mkuu walikubalina kuorodhesha madai yao na kuwasilisha kwake ili kutafuta ufumbuzi wa madai hayo huku wakitupia lawama watendaji wa wizara kuwa hawana nia thabiti ya kutatua madai yao.
Asubuhi na Mapema siku ya Ijumaa Januari 21 ujumbe wa watu watatu ukiongozwa na Rais wa MAT Dk Namala Mkopi,uliwasili Ofisini kwa Pinda na kutoa mapendekezo ya madaktari kutaka kuonana nae.
Hata hivyo safari hii dhamira yao haikutimia baada ya wajumbe hao kuelezwa na wasaidizi wa Pinda kuwa alikuwa safarini kuelekea Arusha.
Wajumbe aho waliwaambia wajumbe wa  mkutano kuwa pamoja na Pinda kuwa safarini kuelekea Arusha bado wangepata jibu la hitaji lao kabla ya saa kumi jioni.
Mwilikilishi wa Pinda awatibua
Huku akionysha hali ya huzuni makamu wa Rais Dk Saidia alisema “Ujumbe uliokwenda kwa pinda umerudi lakini majibu yaliyopatikana huku yamekatisha tamaa washiriki wa mkutano”
Namala alitoa kauli hiyo majira ya saa tatu usiku alipowasiliana kwa njian ya simu na mwanadishi wa makala haya.
Alisema kufautia kauli hiyo washiriki walifikia hatua ya kufanya uamuzi mbya lakini kukafanyika kazi ya ziada ya kuwatuliza.
Alisema pamoja na hatua hiyo wajumbe walikubaliana kukutana tena Jumatatu ya Januari 23 ambapo wangekubaliana hatua za kuchukua.
Siku tanotangu kutangazwa kwa mgomo
Jumanne ya Januri 24 ndio siku ya kwanza ya kuanza kwa mgomo wa madaktari na katika athari zilianza kujitokeza moja kwa moja katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.