Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari.Dk Stephen Ulimboka kabla ya kuanza kwa mkutano wa maridhiano ya kumaliza mgomo wa madaktari,Dk Ulimboka ni
Waziri wa Afya na Usatawi wa Jamii Dk Hadji Mponda
ULIKUWA MGOMO WA KIHISTORIA
Wengi wanasema haijawahi tokea
JANUARI 23 mwaka huu saa 11:30 jioni Dk Stephen Ulimboka mwenyekiti wa jumiya ya Madaktari akatangaza mgomo wa madaktari wenye lengo la kuishinikiza serikali kutekeleza madai yao.
Kutangazwa kwa mgomo kulikofanywa na jumuiya ya hiyo kumekuja baada ya vikao vizito vilivyofanywa na madaktari hao vikongozwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT)kushindwa kuzaa matanda.
Intenship chanzo cha mgogomo
Hilo haliwezi kukwepeka sababu chanzo cha mikutano ya madaktari ilitokana na hatua zilichukuliwa na serikali dhidi ya Madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili kutimuliwa katika vituo vyao vya kazi na kurejeshwa wizarani.
Madaktari hao ambao idadi kamili imekuwa ikishindw kujulikana kufuatia taarifa za awali kudai ni 225 huku habari toka wizarani zikidai ni 197 walitimuliwa na uongozi wa hosptali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwakile kilichoelezwa ni kukiuka mkataba waliongia baina yao na uongozi wa hosptali hiyo.
Mmoja ya vipengele vya mkataba kinaeleza bayana kuwa ni marufuku kwa Interns kugoma wala kushawishi mgomo kwa kipindi chote atakachokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.
Lakini wanataalam hao waligoma kwa muda wa siku mbili mfuliluzo kati ya Januari 3 na 4 wakishinikiza serikali kuwalipa posho zao za miezi miwili zilizokuwa zimecheleweshwa.
Kwa muda wa simu mbili Mgomo uliotangazwa na Jumiya hiyo unadaiwa ni kutokana na hatua zilichukuliwa na lizochukuliwa madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili ambao walitimuliwa na uongozi wa Hosptali hiyo baada ya kuendesha mgomo wa siku mbili wakidai posho zao za miezi miwili.
Idadi ya madaktari hao waliogoma Januari 2 mwaka huu ilikuwa na utata baada ya taarifa za awali zilitolewana uongozi wao kueleza kuwa walikuwa 225 huku tamko la serikali kupitia kwa Naibu waziri wa afya Dk Lucy Nkya ikisema ni 194.
Habari zuilieleza kuwa Madaktari hao walitimuliwa siku moja baada ya kulipw fedha zao ambapo uongozi walipowasili Hosptalini walikumbana na barua iliyowataka kuacha kazi na kurejea Wizarani.
Kufuatia hatua hiyo Junauri 12 mwaka huu Chama cha Maktari Tanzania MAT kiliitisha mkutano wa dhararu wa baraza kuu na kujdali hoja kadhaa huku kikiipa serikali saa 72 kwa serikali kuwarejesha madaktari waliokuwa katika mafunzo katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika tamko lao hilo Madaktari walielezea kuwa kufukuzwa kwa madaktari hao ni ukiukwaji wa haki za binadamu sababu wao walioshindw akuwalipa fedha zao ndio waliotenda kosa na hao ndio waliostahili adhabu
Baraza hilo la dhararua pia lilielezea dhamira ya kuendelea na mkutano wa Madaktari wote siku Juari 18 na kujadili mada mbalimbali ikiwamo ya hatima ya fya ya mtanzania na mazingira bora ya kazi
Majibu ya Wizara
Siku mbili baadaye,Januri 17 Wazira kupitia kwa Naibu waziri wa Afya Dk Lucy Nkya ilitoa tamko lilipuuza madai ya madaktari hao huku likifafanua sababu za kuwatimua katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili kuwa ni kutokana na madaktari hao kuvunja mkataba na mwaajiri wao.
“Ieleweke kuwamba wataalamu hawa huingia mikataba na hosptali husika,mkataba wanaoingia umeainisha kwamba hawatagoma au kuanzisha mgomo”alisema Naibu waziri katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Dk Nkya alifafanua sababu za kuwatawanya katika vituo mbalimbali madaktari hao kuwa ilitokanana tathimini iliyofanywa na wizara ambayo ilibaini kuwapo kwa idadi kubwa ya madaktari wa mafunzo ya vitendo katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika mkutano huo pia Naibu waziri huyo alifafanua kuwa MAT ni miongoni mwa vyama vingine vya hiyari katika sekta ya Afya ambavyo kazi zake ni kufuatilia masuala ya wanachama wao kwa kutumia mifumo iliyowekwa kisheria.
Dk Nkya alisema wataalamu wote katika sekta ya afya katika husimamiwa na mabaraza ya Kitaaluma ambayo ni mamlaka zilizoanzishwa kwa sheria za bunge.
Alisema mabaraza hayo ndiyo yenye dhamana kusimamia ufanisi wa mazoezi kwa vitendo na wahusika huku aitaka MAT kufanya kazi na Wizara iko tayari kushirikiana nao katika masuala yenye kuwezesha kuboresha huduma za afya.
Alionya na kukumbusha chama hicho kutekeleza majukumu yake kwa mjibhu wa katiba ya chama hicho kwa kushirikiana na serikali katika kuimarisha sekta ya afya na wataalamu walio kwenye sekta hiyo kwa manufaa ya nchi badala ya kujihusisha na harakati.
Tamko la Wizara lawatibua Madaktari
Katika mkutano wao wa Januri 18 mwaka huu Madakatari walisema majibu ya Wizara ya kudai madai yao hayana msingi ni ya kisiasa na yakuidhalisha taalamu yao.
Madaktari hao waliokutana katika ukumbi wa Rusian walikubaliana kutuma ujumbe wa watau watatu ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Chama hicho Dk Primus Saidia kwenda wizarani kumuita naibu huyo kwenye mkutano wao.
Hatua ya kumuita Naibu waziri huyo ililenga kupatikana kwa majibu ya maswali yao mengiambayo katika mkutano huo waliibua hoja nne na kuzijadili huku wakieleza kuwa suala la madaktari waliokuwa katikamafunzo ya vitendo lilikuwa linasubiri uamuzi baada ya serikali kushindwa kutekeleza madai yao kwa muda uliokuwa umepangwa.
Ombi la kukutana na Naibu Waziri wa afya
Ujumbe toka Wizarani ulirejea na majibu kuwa Naibu huyo wawaziri alikuwa amekubaru kufika katika ukumbi wa mikutano wao lakini akaomba muda wa saa moja ili aweze kuwasilisna na wasaidizi wake.
Wakati Dk Saidia alikitoa taarifa hiyo,ghafla alipoke simu na kutoka nje ya ukumbi na aliporejea aliwaeleza washiriki wa mkutano zaidi ya 200 waliokuwa wamejipanga kusikiliza naibu waziri huyo na kusema,
“Naibu waziri ameweataka radhi ninyi wote na kueleza kuwa hatakuja kwenye mkutanona badala yake tutakutana nae kesho saa nane mchana”alisema Saidia.
Chenga zikaanza
Siku ya pili ya mkutano Alhamisi ya Januari 19 Madaktari zaidi ya 300 walikusanyika mapema asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Don Bosco wakisubiri ujio wa Naibu waziri huyo wa Afya DK Lucy Nkya.
Wakati wao wakikusanyika ujumbe wa watu watatu ukiongozwa na Makamu wa Rais uliwasilisha barua pamoja na mihitasari ya vikao na madai yao ya jumula na mahali wanapofanyia mkutano.
Wajumbe hao waliporudi walikuja na taarifa za Naibu waziri huyo kukataa kukutana na Madaktari katika ukumbi ulioandaliwa nao na badala yake wizara ingeandaa ukumbi mwingine.
Madaktari walipinga kitendo hicho kwa madai kuwa kilikuwa ni matumizi mabaya ya fedha sababu wao walikuwa tayari wamelipia ukumbi huo,lakini pia wakadai tukio hilo lingesababisha usumbufu kwao.
Wakiwa bado kwenye chumba hicho madaktari hao ghafla walielezwa tayari ukumbi ulikuwa umepatikana ambao ni Arnatoglo na kuwataka wao kwenda katika ukumbi huo kwa muda wa nusu saa vinginevyo Waziri huyo na ujumbe wake angeondoka.
Madaktari waligoma kwenda kwenye ukumbi huo kwa kile walichodai kuwa ni umbali wa kutoka eneo walipo na kwamba kutokana na hali ya usafiri ilivyokuwa muda wa nusu saa usingetosha kumkuta DK Nkya akiwa kwenye chumba cha mkutano.
Pia Dk Saidia alisema kundi la madaktari hao lingeonyesha taswira ya maandamano jambo ambalo lingesababisha usumbufu kwa wananchi wanaotumia njia hizo na pia kuhofia uwezekano wa Madaktari hao kukamatwa na Polisi kwa kisingizio cha kuandamana bila kibali.
Aidha madaktari hao wakasema Naibu waziri huyo ameonyesha dhararu kwa kitendo chake cha kwenda ukumbi mwingine ilihali akijua watu wako sehemu nyingine.
“Nirahisi kwa yeye kuja kuliko umati wa watu 300 kujaa barabarani kwa lengo la kumfuata,lakini kwanini ameenda Arnatouglo hali akijua watu wako huku,hii ni dhararu”alisema mmoja wa madaktari alipochangia kwenye mkutano wao.
Kufuatia mvutano huo Madaktari waligoma na kuweka azimoa la kukutana siku ya pili katika mwenndelezo wa mkutano wao huku wakiwa na wazo la kuona mamlaka nyingine za juu.
Kwa upande wake kutokana na mvutano huo Dk Nkya alikaririwa na vyombo vya habri akisema asingewasikiliza tena Madaktari na kuwataka madai yao yafikishwe serikalini kwa kutumia Shirikisho la vyama vya Serikali kuu na Afya (TUGHE) ambao wapo kisheria kushughulikia madai hayo.
"Madaktari hawa wameonyesha kiburi,kuanzia sasa sitawasikiliza na badala yake madai yao yote yawasilishwe wizarani kupitia Tughe na kama wataaendelea na vikao vyoa mfululizo kwa siku saba nitawafukuza"anasema Dk Nkya.
Harakati za kumona Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Siku iliyofuata Madaktari hao walikutana tena katika ukumbi wa mikutano wa Don Bosco na kudhamilia kumuona Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Madaktari huku wakiwa na imani kubwa na Waziri Mkuu walikubalina kuorodhesha madai yao na kuwasilisha kwake ili kutafuta ufumbuzi wa madai hayo huku wakitupia lawama watendaji wa wizara kuwa hawana nia thabiti ya kutatua madai yao.
Asubuhi na Mapema siku ya Ijumaa Januari 21 ujumbe wa watu watatu ukiongozwa na Rais wa MAT Dk Namala Mkopi,uliwasili Ofisini kwa Pinda na kutoa mapendekezo ya madaktari kutaka kuonana nae.
Hata hivyo safari hii dhamira yao haikutimia baada ya wajumbe hao kuelezwa na wasaidizi wa Pinda kuwa alikuwa safarini kuelekea Arusha.
Wajumbe aho waliwaambia wajumbe wa mkutano kuwa pamoja na Pinda kuwa safarini kuelekea Arusha bado wangepata jibu la hitaji lao kabla ya saa kumi jioni.
Mwilikilishi wa Pinda awatibua
Huku akionysha hali ya huzuni makamu wa Rais Dk Saidia alisema “Ujumbe uliokwenda kwa pinda umerudi lakini majibu yaliyopatikana huku yamekatisha tamaa washiriki wa mkutano”
Namala alitoa kauli hiyo majira ya saa tatu usiku alipowasiliana kwa njian ya simu na mwanadishi wa makala haya.
Alisema kufautia kauli hiyo washiriki walifikia hatua ya kufanya uamuzi mbya lakini kukafanyika kazi ya ziada ya kuwatuliza.
Alisema pamoja na hatua hiyo wajumbe walikubaliana kukutana tena Jumatatu ya Januari 23 ambapo wangekubaliana hatua za kuchukua.
Siku tanotangu kutangazwa kwa mgomo
Jumanne ya Januri 24 ndio siku ya kwanza ya kuanza kwa mgomo wa madaktari na katika athari zilianza kujitokeza moja kwa moja katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.