Iringa.Kijana Frenk Kiwele
anayekabiliwa na tatizo la kutokwa na haja kubwa na ndogo mfulilizo amepkea
msaada wa Sh 510,000 kutoka kwa wasomaji wa gazeti la Mwananchi na kudai sasa
anapata matumaini ya kupona tatizo lake.
Kiwele alikabidhiwa fedha hizo juzi
na mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani hapa
Geofrey Nyang’oro ambaye pia ndiye mmiliki wa mtandao huu,hafla hiyon
amefanyika nyumbani kwake Kinegamgosi A
kata ya Ruaha ndani ya Mansipaa ya Iringa.
Hafla hiyo imeshuhudiwa na Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu wa Manispaa ya
Iringa Gasper Nsanye na Mjomba wa kijana huyo Thomas Ngandango.
Akizungumza muda mufi baada ya
kukabidhiwa fedha hizo Frank aliwashukuru
wasomaji wa Gazeti hilo kwa kumchangia
kiasi hicho cha fedha baada ya kusoma makala hiyo licha ya kuwa hawamjui na
kudai mungu atawazidisha pale walipopungukiwa.
Kwa mjibu wa taarifa ya madakati Bingwa kutoka
Hosptali ya Taifa ya Muhimbili waliofanya uchunguzi wa tatizo lake wanadai
gharama zinazohitajika kwa ajili ya matibabu ya Farnk Kiwele ni Sh 3,650,750
Kwa upande wake Afisa Usitawi wa
Jamii Mkuu wa Manispaa ya Iringa Gasper Nsanye amemshukuru mwandishi wa makala
hayo, kampuni ya Mwananchi Communicationi LTD ambao ni wachapishaji wa magazeti
ya Mwananchi,Thecitizen na Mwanaspoti kwa kukubali kuchapisha makala hayao gazeti jambo
liliwafanya wasomaji wake kuoisoma na kutoa kiasi hicho cha fedha.
“Mini nianze kwa kumshukuru mwandishi wa
makala haya,nilishukuru kampuni ya Mwananchi Communication LTD na pia wasomaji
wa gazeti la Mwananchi kwa mchango wao,ofisi yetu inashughulikia suala hilo kw
akaribu na hivi sasa tumefungua kitabu cha Benki katikA Benki ya NMB chenye
akaunti namba ya FRANK ELIUTA KIWELE A/C
NO 16110000481”alisema Nsanye na kuongeza:
“Katika A/C hiyo kwenye kikao cha
wakuu wa Idara na waheshimiw amadiwani wa Manispaa ya Iringa walichangia Sh
150,000 huku wadau wengine wa mkoani hapa wakitoa mchangia wa Sh 50 000 na
kufanya jumla ya Sh 200,000 na kwa sasa tukichanganya na hizo tutakuwa na Sh
700,000”alisema Nsanye.
Nsanye alisema bado michango
inahitajika kufikia kiwango kinachohitajika na kuongeza kuwa hata uongozi wa
Manispaa hiyo unaendelea na mchakato wa kuwafikia wadau mbalimbali kwa ajili ya
kufanikisha jukumu hilo.
Naye Mjumba wa Frank Thomas alitoa
shukurani zake kwa makundi yote yalitoa mchango huo na kudai pindi kiasi hicho
kitakapopatikana atakuwa bega kwa bega katika kuuguza mpya wake kazi
aliyoifanya kw amda mrefu sasa.
MWISHO